Rostam: Hatuwezi kufanikiwa kwa kuwatenga wafanyabiashara wa ndani na kutegemea wageni

Na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA maarufu na mwakilishi wa sekta binafsi, Rostam Azizi, amesema kuwa mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 hayawezi kufikiwa kama taifa halitawalinda na kuwawezesha wafanyabiashara wa Kitanzania.

Akizungumza leo Julai 17, 2025 katika hafla ya uzinduzi wa Dira hiyo jijini Dodoma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rostam amesema ni lazima Watanzania wawe sehemu kubwa na muhimu ya uchumi wao.

“Hatutafanikisha haya yote bila kuwalinda, kuwatetea na kuwasaidia wafanyabiashara wa Kitanzania. Hamna nchi duniani iliyojengwa na wageni,” amesisitiza Rostam, akihimiza serikali kuweka sera, sheria na mifumo ya kifedha inayowabeba Watanzania.

Rostam amesisitiza kuwa manunuzi ya serikali na zabuni zipewe kwa upendeleo mzuri kwa wazawa, huku akitaka mabadiliko ya haraka katika sekta ya kifedha ili kurahisisha upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali wa ndani.

Ameongeza kuwa mfumo wa kibenki wa sasa hauwapi nafasi wafanyabiashara wa Kitanzania kukua.

Akimpongeza Rais Samia kwa uongozi wake wa miaka minne, Rostam amesema serikali yake imejenga msingi imara kwa Dira ya 2050 kupitia uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya usafiri, nishati, maji na nidhamu ya utekelezaji wa miradi ya kitaifa.

“Umeua kasumba ya kila kiongozi kuanza upya na kupuuza miradi ya mtangulizi wake. Umeweka msingi wa kizalendo katika uongozi,” amesema.

Rostam pia amesisitiza kuwa Dira 2050 si ya serikali pekee bali ni ya taifa zima, na utekelezaji wake unahitaji ushirikiano wa dhati kati ya sekta ya umma na binafsi.

Alipongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uundaji wa Dira hiyo, akisema maoni yao yalisikilizwa na kutekelezwa.

Aidha ametaka kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vipaji utakaoandaa vijana wa Kitanzania kuwa wabobezi katika maeneo ya kimkakati kama akili bandia, uhandisi, na fedha, na kuwatumia kama rasilimali hai kwa maendeleo ya taifa.

Rostam ametoa wito kwa Tume ya Mipango kuongoza mageuzi hayo kwa maono, weledi na dhamira ya kweli ya kulijenga taifa lenye ushindani wa kimataifa.

“Huu ni wakati wetu wa kusonga mbele kwa uthubutu. Sekta binafsi ipo tayari,” amesema.

spot_img

Latest articles

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria...

More like this

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...