Prof. Kabudi: Anayefanya kazi bila ‘Press Card’ anavunja Sheria

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amesema yeyote anayefanya kazi za kihabari bila kuwa na Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) kinachotolewa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB anavunja sheria ya Huduma za Habari.

Waziri Kabudi ametoa kauli hiyo huku akionesha Press Card yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mabaraza ya Habari Afrika, Julai 14, 2025 alipozungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango jijini Arusha.

Amesema Press Card aliyopewa siyo kwa hisani bali ni kutokana na kukidhi vigezo, akiwa amewasilisha vyeti vya taaluma ya Uandishi wa Habari kwenye mfumo wa Bodi, huku akiwasisitiza Waandishi wengine kujisajili katika mfumo wa TAI-HABARI.

Waziri Kabudi amemuhoji Katibu Mtendaji Mstaafu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambao ni wenyeji wa Mkutano huo, Kajubi Mukajanga kama ameshajisajili na kupata Press Card, ambapo amekiri kuwa bado lakini atafanya hivyo siku chache zijazo nyaraka zake zikikamilika.

Mkutano wa Mabaraza la Habari Afrika unafanyika kwa mwaka wa pili nchini Tanzania ukitanguliwa na Mkutano wa kwanza uliofanyika Mwaka jana nchini Afrika Kusini.

spot_img

Latest articles

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria...

More like this

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...