Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Fountain Gate imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa mtoano uliopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, mkoani Manyara.
Fountain Gate meshinda jumla ya mabao 5-1 katika michezo miwili ya mtoano ya nyumbani na ugenini baada ya kushinda 3-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na leo wakahitimisha kwa ushindi wa 2-0 nyumbani.
Mabao ya leo yamefungwa na Elie Mkono dakika ya 51 na Edger William dakika ya 90, hivyo kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kuendelea kusalia kwa msimu wa 2025/2026.
Ushindi huo umeleta furaha kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na kukwepa kushuka daraja kupitia hatua ya mtoano.