Wafanyakazi wa Majumbani 700 Watunukiwa Vyeti vya Mafunzo ya VETA

Na Tatu Mohamed

ZAIDI ya wafanyakazi wa majumbani 700 wamepatiwa mafunzo maalum na kutunukiwa vyeti na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kwa lengo la kuwawezesha kupata ujuzi mahususi kwa kazi zao.

Kwa mujibu wa Muwezeshaji wa mradi huo, Debora Mwageni, mafunzo hayo yanamwezesha mfanyakazi wa ndani kuwa na uwezo wa kushiriki majadiliano yenye lengo la kuboresha mazingira ya kazi pamoja na kupata maslahi bora.

Akizungumza katika banda lao kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2025, Debora amesema mradi huo ulianza Aprili mwaka jana na umepokelewa kwa muitikio mkubwa.

“Wafanyakazi wa ndani wanasaidiwa kuelewa majukumu yao, haki na wajibu wao katika kazi wanazofanya,” amesema.

Aidha, amesema kupitia mradi huo, wafanyakazi hao wanawezeshwa kupata ajira za kudumu, kulinda afya zao na kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama.

Mafunzo hayo yanahusisha masuala mbalimbali kama vile uandaaji wa chakula, usimamizi wa nyumba, usafi, kufua na kunyoosha nguo, pamoja na malezi ya watoto na wazee.

Debora ameongeza kuwa mafunzo pia yanawaandaa kwa ajili ya kufanya kazi katika nchi za nje kama vile Dubai, Oman, Denmark, Uingereza, Marekani na Italia.

“Tunawapa ujuzi wa stadi za maisha, elimu ya afya ya uzazi, pamoja na mbinu bora za kuwahudumia watu wanaoishi nao kwa ukarimu huku wakifahamu haki zao za msingi,” amesema.

Ameeleza kuwa wafanyakazi wa ndani ni sawa na wafanyakazi wengine, hivyo wanapaswa kupata heshima stahiki na kutambuliwa rasmi.

Debora amewashauri Watanzania kujiwekea utamaduni wa kupata elimu na mafunzo kabla ya kuajiriwa ili kujiimarisha katika kazi zao.

spot_img

Latest articles

TPDC Yahimiza Wananchi Kulinda Miundombinu ya Bomba la Gesi Asilia

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuwashirikisha wananchi...

TMA yatangaza msimu wa Kipupwe Juni hadi Agosti

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kuwa na msimu...

Kamati ya Bunge yaridhishwa na uzalishaji wa kiwanda cha sukari Mkulazi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeendelea kutekeleza mikakati iliyoanishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050...

Wachina wanne wakamatwa kwa utekaji

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia raia wanne...

More like this