Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ‘Sabasaba’ kutangaza hudumaDar es Salaam.

Ofisi ya Msajili wa Hazina imetoa rai kwa taasisi za umma kutumia maonesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba kama jukwaa la kutangaza huduma zinazotolewa na serikali.

Akizungumza Jumatatu, Julai 1, 2025, katika viwanja vya Sabasaba, Sabato Kosuri, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, amesema wananchi ndio wamiliki wa taasisi za umma na hivyo wanahaki ya kujua uwekezaji uliofanyika.

Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imewekeza kiasi cha Sh86.25 trilioni katika taasisi za umma na kampuni ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache.

Kati ya kiasi hicho Sh83.33 trilioni zimewekezwa kwenye taasisi 152 ambazo serikali ina hisa nyingi, huku Sh2.82 trilioni zikiwekezwa kwenye kampuni 56 ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache.

Kosuri amesema Maonesho ya biashara ya Sabasaba ni mwendelezo wa tafsiri ya ndoto ya Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuongeza ufanisi wa taasisi za umma lengo likiwa ni kuleta tija na rejesho halisi la uwekezaji uliofanywa katika taasisi za umma.

“Sisi kama wasaidizi wa Mhe. Rais tumedhamiria kutengeneza mazingira ya uwajibikaji kwani taasisi za umma ni mali za umma na hivyo zinawajibika moja kwa moja kwa umma,” amesema.

Kosuri amesema ushiriki wa Ofisi ya Msajili wa Hazina na taasisi inazozisimamia katika maonesho ya Sabasaba utawapa fursa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuuliza maswali na kutoa maoni.

“Tutumie maonesho ya Sabasaba kama jukwaa la kupokea maoni na kuwaambia wadau na wananchi kwa ujumla mambo ambayo serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais. Dk. Samia Suluhu Hassan inayafanya,” amesema Kosuri.

Amewakaribisha wadau mbalimbali na wananchi wote katika banda namba 39 la Ofisi ya Msajili wa Hazina lililopo katika ukumbi wa Kilimanjaro.

spot_img

Latest articles

Makofi, vigelegele vimemrarua Mwigulu Nchemba?

Na Jesse Kwayu KATIKA mfumo wa utawala ambao chimbuko la madaraka ya dola ni wananchi,...

DCEA yakamata Tani 9.93 za Dawa za Kulevya, Watuhumiwa 151 Watiwa Mbaroni

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata tani...

Media Brains yaendesha mafunzo kwa wanahabari kutumia dijitali

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wanaendesha mafunzo...

Msajili wa Hazina afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Lifezone Metal

Na Mwandishi wa OMH Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amefanya mazungumzo na Bw. Keith Liddell,...

More like this

Makofi, vigelegele vimemrarua Mwigulu Nchemba?

Na Jesse Kwayu KATIKA mfumo wa utawala ambao chimbuko la madaraka ya dola ni wananchi,...

DCEA yakamata Tani 9.93 za Dawa za Kulevya, Watuhumiwa 151 Watiwa Mbaroni

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata tani...

Media Brains yaendesha mafunzo kwa wanahabari kutumia dijitali

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wanaendesha mafunzo...