Rais Mwinyi aipongeza Yanga, aizawadia  milioni 100

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Klabu ya Yanga  Sh 100 milioni  kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa waliopata katika msimu wa mwaka 2024/2025.

Rais  Mwinyi ameyasema hayo leo Juni 30, 2025 alipokutana na viongozi pamoja na wachezaji wa Yanga waliofika Ikulu  Zanzibar kwa ajili ya kumkabidhi makombe matano ya michuano mbalimbali waliyoyatwaa msimu huu.

Amepongeza mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana na klabu hiyo kongwe, akieleza kuwa yanajenga heshima na historia muhimu katika tasnia ya michezo nchini.

Aidha, ameishukuru klabu hiyo  kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi kupitia kampeni ya Visit Zanzibar, huku akieleza kuwa hatua ya klabu hiyo kucheza baadhi ya michezo yake Zanzibar kunachangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni na wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.

Halikadhalika, Rais Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha viwanja vya michezo ili kuwezesha michuano mingi zaidi kufanyika Zanzibar.

Naye Rais wa Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vilabu vya Soka Barani Afrika, Hersi Said, amemkabidhi Rais Mwinyi medali maalum ya michuano ya CRDB  pamoja na jezi ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kutoa pongezi na shukrani kwa Rais  kutokana na  juhudi zake za kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuahidi kuwa klabu hiyo itaendelea kucheza mechi zake visiwani humo.

Katika msimu wa 2024/2025 Yanga  imefanikiwa kutwaa makombe  matano ambayo ni Ngao ya Jamii, Kombe la Michuano ya Toyota, Kombe la Muungano, Kombe la Ligi Kuu  Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho.

Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Dar es Salaam, huku kikipokewa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo, wakishudia makombe yote matano yakiwa kwenye gari maalum.

spot_img

Latest articles

Makamu wa Rais atoa wito uboreshaji mfumo wa fedha

Na Mwandishi Wetu Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango ametoa wito wa kufanyika maboresho ya...

Esther Bulaya: Nilikuwa Chadema kwa mkopo nimerejea, CCM ni kama  Barcelona 

Na Mwandishi Wetu Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Kihongosi aahidi kutekeleza alichoagizwa na Rais Samia  Arusha

Na Mwandishi Wetu  Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha,  Kenani Kihongosi amesema  atafanya kazi aliyotumwa na Rais...

Israel Salufu wa CCM achukua fomu ya kuwania Jimbo la Kilolo

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Israel Johaness Salufu amechukua fomu kuwania nafasi ya...

More like this