Bondia Debora amtangazia vita Asia, apania kulipa kisasi

Na Winfrida Mtoi

Bondia  wa ngumi za kulipwa nchini, Debora Mwenda, ametangaza vita dhidi ya mpinzani wake Asia Meshack , akiahidi kulipa kisasi katika pambano la Dar Boxing Derby litakalofanyika Julai 26, 2025, jijini Dar es Salaam.

Amesema  pambano lililopita baada ya kupoteza alipata hasira kali hadi kulia ulingoni, hivyo bado ana machungu na hasira zote atazimaliza  mchezo ujao watakapokutana  tena na mpinzani wake.

“Nimuambie tu mpinzani wangu Asia kuwa bado nina hasira  ya mechi niliopoteza mbele yake na  nililia.  Namuambia ajipange maana hiyo hasira iliyonifanya ya nilie itakuja kumuishia yeye,” ametamba Debora.

Amesema mashabiki wake watarajie kuona mabadiliko ulingoni kwa kuwa amejipanga kuwapa burudani na kuondoka na ushini siku hiyo.

Hata hivyo amekiri kuwa mpinzani wake ni mzuri lakini amejiandaa vizuri kuhakikisha hawezi kurudia makosa yaliyomfanya apoteze pambano lililopita.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this