Rais Mwinyi kuvunja Baraza la Wawakilishi Agosti 13

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza kuwa atalivunja rasmi Baraza la Kumi la Wawakilishi ifikapo  Agosti 13, 2025.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichofanyika leo Juni  23,2025, Chukwani, Mkoa wa Mjini Magharibi,amesema kuwa hatua hiyo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 92 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Katika hotuba yake, Rais Dk. Mwinyi ameelezea kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake ni pamoja na kuimarika kwa uchumi, kuendelezwa kwa amani, na mafanikio ya kuwaleta wananchi pamoja bila kujali rangi, asili, jinsia, dini au itikadi za kisiasa. Pia amesisitiza kuendelea kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kuhusiana na Muungano, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa mafanikio yamepatikana katika kuimarisha Muungano wa Tanzania kisiasa, kiuchumi na kijamii, tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kushughulikia hoja za Muungano mwaka 2006, ambapo hoja 26 zimejadiliwa na 22 kupatiwa ufumbuzi.

Akihitimisha hotuba yake,  amewasisitiza wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kushiriki uchaguzi kwa kudumisha amani kabla, wakati, na baada ya uchaguzi. Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa, asasi za kiraia na viongozi wa dini kutekeleza wajibu wao wa kikatiba katika kipindi hiki muhimu.

Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) kupitia Tume za Uchaguzi za ZEC na NEC, inaendelea na maandalizi ya uchaguzi kwa misingi ya haki na sheria.

Mapema, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, alitangaza rasmi kumalizika kwa maisha ya Baraza la Kumi la Wawakilishi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kumshukuru Rais wa Zanzibar kwa ushirikiano wake pamoja na kuwashukuru wajumbe wa Baraza kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...