Kinyozi ahukumiwa  kifungo cha miaka 30 jela kwa kubaka mwanafunzi

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Wilaya ya Kwimba imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela kinyozi wa saluni ya kiume, Lindwa Clement Balthazari (30), mkazi wa kijiji cha Malya  baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 kutoka Shule ya Msingi Mwakulilima.

Hukumu hiyo imesomwa leo, Juni 17, 2025, na Hakimu Mkazi Mfawidhi Ndeko Dastan katika kesi ya jinai namba 31961/2024, baada ya mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desemba 4, 2024, na kusomewa shtaka la kubaka na Wakili wa Serikali Juma Kiparo, ambapo alikana kutenda kosa hilo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Lindwa alitenda kosa hilo nyumbani kwake kwa nyakati tofauti mwezi Oktoba 2024, akitumia nafasi ya kumhudumia mtoto huyo kwenye saluni yake kabla ya kumrubuni na kumbaka, kinyume na vifungu vya sheria 130(1), 130(2)(e), na 131(1) vya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (marejeo ya 2022).

Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi wanne, wakiwemo mhanga na daktari, kuthibitisha pasipo shaka tuhuma hizo. Mtuhumiwa alijitetea kuwa alimchukua binti huyo kwa lengo la kumsaidia baada ya kufukuzwa nyumbani, hoja ambayo ilitupiliwa mbali na Mahakama.

Jitihada zake za kuleta mashahidi watatu kwa ajili ya utetezi hazikufua dafu, na Mahakama ikamhukumu kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

More like this