Media Brains yaandaa waandishi wa habari kwa uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Waandishi wa habari mkoani Kigoma wamepewa mafunzo ya kuwasadaia kuandika vema habari za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Mafunzo hayo yanayotolewa na kampuni ya masuala ya habari ya Media Brains yanalenga kuwajengea waandishi wa habari uelewa wa sheria zinazohusu uchaguzi, pamoja na kuwaelekeza njia sahihi za kuripoti habari hizo.

Mafunzo hayo yanayodhaminiwa na shirika lisilo la kiserikali la Konrad Adenaeur Stiftung (KAS), yanahusisha kujenga uelewa wa sheria tatu zinazogusa uchaguzi mkuu. Sheria hizo ni ya vyama vya siasa; sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani na sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa (INEC).

Akitoa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mwenza wa Media Brains ambaye pia ni mwandishi wa habari nguli nchini, Absalom Kibanda, aliwataka waandishi hao kujibidiisha kusoma sheria hizo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuripoti uchaguzi kwa usahihi.

“Someni hizi sheria vizuri. Jijengeeni uwezo wa kuzitambua vema ili ziwaongoze katika kazi zenu. Hizi sheria zimepitishwa miaka ya hivi karibuni na zimekwisha kuanza kutumika katika mchakato wa awali wa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu,” alisema Kibanda.

Aliwakumbusha waandishi kwamba pamoja na ukweli kwamba mabadiliko ya sheria hizo, hasa ile inayounda INEC imeweka utaratibu bora zaidi wa kupata wajumbe wa uchaguzi kuliko ilivyokuwa zama za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Media Brains, Jesse Kwayu, aliwakumbusha waandishi wa habari juu ya kuzingatia usawa wa kijinsia katika kuandika habari za uchaguzi mkuu.

Ripoti na tafiti zilizofanyika hapa nchini zinaonyesha kwamba vyombo vya habari huwabagua wagombea wanawake na kuwapa upendeleo wanaume.

“Ripoti ya jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti uchaguzi mkuu wa 2020 iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, inaonyesha kuwapo kwa upendeleo mkubwa kwa wagombea wanaume dhidi wanawake,” alisema Kwayu.

Akizungumza katika mafunzo hayo ya siku moja, Mkurugenzi wa Media Brains, Neville Meena, aliwaakumbusha waandishi kuwa wakiweka bidii kuzifahamu sheria za uchaguzi itawarahisishia kazi zao, hasa wanapowahoji wagombea na wadau wengine wa uchaguzi hasa katika madai ya kuwapo kwa sheria kandamizi na zisizo rafiki katika uchaguzi.

“Ukiwa unazifahamu sheria, wakati unahoji watu wanaotoa changamoto kama za uhuru wa INEC utakuwa na uwezo wa kuuliza mambo ya msingi ili kupata hasa undani na ukweli wa madai yao,” alisema.

spot_img

Latest articles

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria...

More like this

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...