Waziri wa Mazingira wa Norway ateta na Waziri Masauni

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mha. Hamad Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na Andreas Bjelland Eriksen – Waziri wa Hali ya Hewa na Mazingira wa Norway.

Mazungumzo hayo yalilenga ushiriki wa Tanzania katika COP30 na majadiliano kuhusu taka za Plastiki, yalifanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Oslo, nchini Norway.

Akizungumza kuhusu jitihada za Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi, Waziri Masauni alimweleza Eriksen kuwa Tanzania imejipanga kuhifadhi Mazingira kwa kuja na mipango na makatazo mbalimbali ikiwepo agenda ya Nishati Safi ya kupikia.

Tanzania imepanga kupunguza matumizi ya Nishati isiyo salama ya kupikia na kuhakikisha kuwa kufikia 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wakitumia nishati Safi ya Kupikia.

Aidha Waziri Masauji, alimweleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika na Duniani kote.

Waziri Masauni aliendelea kuelezea kuwa Tanzania imekuwa na program za mpito kwa kutoa makatazo ya matumizi ya kuni na mkaa kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kuanzia 2024.

Aidha Tanzania imetoa katazo la matumizi ya plastiki (Vibebeo) na kuainisha tofauti ya vibebeo na vifungashio.

Akizungumza Waziri Eriksen amesema kuwa COP30 ni fursa adhimu kwani kila nchi duniani itapata fursa ya kuwasilisha taarifa yake ya tatu ya ‘Nationa Determined Contribution’-NDC.

“Nina imani kuwa pamoja na taarifa hizo kuna baadhi ya nchi zitakuwa zimetimiza adhma zao na baadhi kutotimiza hivyo COP30 itatoa fursa ya kuona nini kifanyike ili kuziba mapengo hayo”, amesema Eriksen.

Aidha ameleza kuwa kwa kufanya kazi kwa mashirikiano baina ya mataifa mbalimbali ni matarajio yake kuwa ahadi ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi- ‘Adaptation Finance’ itaongezeka mara tatu – ‘Triplering Adaptation fund’.

Serikali ya Norway inafanyia kazi upatikanaji wa fedha kwa ajili ya masuala ya Mazingira na tayari wana Mfumo wa utekelezaji wa Artice 6 ambao unawasaidia katika utekelezaji wa miradi jumuishi, ili kuwa na lengo la pamoja na hivyo kuibua fursa mpya.Article 6 inalenga kuibua fursa mpya.

Hivyo Tanzania ikiwa mwenyekiti wa ‘ African Group of Negotiators’- AGN inaweza tumia fursa hiyo kuzishawishi nchi hizo kutambua fursa zilizopo na kuzitumia kwa mapana zaidi.

Akizungumzia taka za plastic Waziri Eriksen ameeleza kuwa kuna umuhimu wa majadiliano ya kina kuhusu taka za plastiki kwani zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku.

Hivyo ni muhimu mataifa yakashirikiana kukabiliana na janga hili.

spot_img

Latest articles

Rukwa mbioni kunufaika na umeme wa Gridi ya Taifa baada ya kukamilika kwa Mradi wa TAZA

📌 Utekelezaji Mradi wa TAZA wafikia asilimia 95 📌 Ili kuukamilisha mradi kutakuwa na katizo...

Mradi wa Kurasini Logistics Park wakamilika kwa asilimia 90

Na Tatu Mohamed MRADI wa ujenzi wa Kurasini Logistics Park katika Bandari Kavu ya EPZA,...

WAZIRI HOMERA AMPONGEZA RAIS SAMIA KUONGOZA KWA VITENDO AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA BARANI AFRIKA

📌Ataja matumizi ya nishati safi kupanda kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia...

HAKIKISHENI MNAMBANA MKANDARASI ILI MRADI WA UMEME SONGEA – MASASI UKAMILIKE KWA WAKATI – MHE. NDEJEMBI

📌Akagua Mradi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa Kv 220 Songea...

More like this

Rukwa mbioni kunufaika na umeme wa Gridi ya Taifa baada ya kukamilika kwa Mradi wa TAZA

📌 Utekelezaji Mradi wa TAZA wafikia asilimia 95 📌 Ili kuukamilisha mradi kutakuwa na katizo...

Mradi wa Kurasini Logistics Park wakamilika kwa asilimia 90

Na Tatu Mohamed MRADI wa ujenzi wa Kurasini Logistics Park katika Bandari Kavu ya EPZA,...

WAZIRI HOMERA AMPONGEZA RAIS SAMIA KUONGOZA KWA VITENDO AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA BARANI AFRIKA

📌Ataja matumizi ya nishati safi kupanda kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia...