Upanuzi wa Kituo cha Kupoza umeme Mbagala mbioni kukamilika

📌Awamu ya kwanza ya upanuzi wa Kituo Megawati 45 yakamilika

📌Asema wananchi wa Mbagala na Temeke watapata umeme wa uhakika

📌Awataka wananchi wa Mbagala kuendelea kuwa wavumilivu wakati wa utekelezaji wa Mradi

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Twange amesema wananchi wa maeneo ya Mbagala na viunga vyake sasa wanatarajia kupata umeme wa uhakika baada ya Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala kuongezewa uwezo kutoka Megawati 45 za awali na kufikia Megawati 165.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kituo hicho, Twange alisema kuwa Kituo hicho kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali hivyo kitakuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza umeme na kuondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa umeme katika maeneo hayo.

“Kituo hiki kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali na mpaka sasa utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia 70. Wananchi wa Mbagala na viunga vyake sasa wategemee umeme wa uhakika’’ amesisitiza Twange.

Pia, Mkurugenzi Mtendaji, Lazaro amemshukuru sana Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani milioni 6.4 ili kufanikisha Mradi huu wenye tija na manufaa kwa wananchi wa maeneo hayo na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda, akizungumza wakati wa ziara hiyo amepongeza jitihada zinazofanywa na TANESCO ambapo amefafanua kuwa kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kumaliza kero ya umeme katika maeneo mengi ya Mbagala, Temeke na Mkuranga.

“Kwa namna ya pekee tunaishukuru sana TANESCO kwa mradi huu, kwa awamu ya kwanza Mradi huu ulipaswa kujaribiwa mwezi Juni mwaka huu lakini Mradi umeweza kuonesha mafanikio kabla ya wakati kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa’’ alifafanua Mapunda.

Uboreshaji wa Mradi huu wa Kituo cha Kupokea na Kupoza na Kusambaza umeme cha Mbagala umegharimu Dola za Kimarekani milioni 6.4 ambapo sasa umefikia asilimia 70 ya utekelezaji wake na kukamilika kwake kunatarajia kusambaza umeme wa Megawati 165.

spot_img

Latest articles

Rostam Aziz ainunua Nation Media ya Kenya

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taarifa Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz imeingia makubaliano ya...

Mwili wa Mwanahabari Mkongwe Makaranga waagwa Dar, kuzikwa Mwanza

Na Mwandishi Wetu WAANDISHI wa Habari, Wahariri, ndugu na jamaa leo Machi 10, 2026, wamejumuika...

Wanawake TRA Wapongezwa kwa Mchango wa Ukusanyaji Mapato

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, amewapongeza wanawake wa...

Mchungaji Kimaro: Miradi ya Familia Ndio Suluhisho la Ajira kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu  MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjiri Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama Dk....

More like this

Rostam Aziz ainunua Nation Media ya Kenya

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taarifa Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz imeingia makubaliano ya...

Mwili wa Mwanahabari Mkongwe Makaranga waagwa Dar, kuzikwa Mwanza

Na Mwandishi Wetu WAANDISHI wa Habari, Wahariri, ndugu na jamaa leo Machi 10, 2026, wamejumuika...

Wanawake TRA Wapongezwa kwa Mchango wa Ukusanyaji Mapato

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, amewapongeza wanawake wa...