TFF kuja mshirika wa kubashiri mechi zake

Na Mwandishi Wetu

Shirikisho wa Soka Tanzania(TFF),limesema kuanzia msimu ujao wa 2025/2026 litakuwa na mshirika wa michezo ya kubashiri(kubeti) katika mashindano yake yote.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF  waliyotoa leo, Mei 12, 2025 mshirika huyo atashikilia haki hizo kwa kipindi chote cha makubaliano, hivyo yeyote mwenye nia au kuhitaji ‘Odds’ kwa ajili ya mechi ambazo zitakuwa chini ya TFF atalazimika kuwasiliana na mshirika huyo.

“Makubaliano yetu na mshirika huyo yatakuwa ni kwa ajili ya odds tu na si ushirika mwingine na kampuni za michezo ya kubashiri(betting companies) kama udhamini(sponsorship) au ushirikiano,” imesema taarifa hiyo kwa umma.

Taarifa hiyo imesema kuwa utaratibu huo ndio unaotumika katika ligi mbalimbali barani Ulaya, ikieleza kuwa itazinufaisha kimapato klabu mechi zao zitakuwa zimeingia kwenye odds.

“Licha ya malipo yatakayokuwa yanatokana na odds, bado klabu zitaendelea kudhaminiwa na kampuni hizo michezo ya kubashiri, kwani utaratibu huu hauathiri makubaliano ya udhamini kati ya pande hizo.

“Utaratibu wa kumpata mshirika huyo utafanyika kwa njia ya mnada utakaotangazwa  wakati wa utakapowadia,” imesema.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this