Serikali yatambua mchango wa Kibanda katika tasnia ya habari, yampa zawadi

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Mwandishi wa Habari Mkongwe,  Absalom Kibanda ambaye pia ni Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Media Brains,  amezawadiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokana na mchango wake katika tasnia ya habari nchini.

Zawadi hiyo ya fedha taslimu Sh 10 milioni, imekabidhiwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa utoaji tuzo za Samia  Kalamu  Awards 2025, jijini Dar es Salaam.

Kibanda amepewa zawadi hiyo pamoja na wakongwe wengine ambao ni Deodatus Balile, Haula Shamte na Baraka Islam  kutokana na uandishi wao mahiri wa habari na uchambuzi hasa katika masuala ya siasa.

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi hizo, Prof. Kabudi amesema habari na makala ambazo wameziandika wakongwe  hao zimekuwa mchango mkubwa na zimewaleta watanzania pamoja bila kuligawa Taifa.

“Mheshimiwa Rais nawiwa wingi wa shukrani kwa  waandishi wenzangu wa habari, na wapo  waandishi wa habari mahiri wa habari za siasa zenye uchambuzi wa kina, zinazojenga umoja, uzalendo, mshikamano na zinazotambua hatua kubwa za kimaendeleo ambayo Taifa letu limepga hasa katika miaka hii minne ya uongozi wako.

“Habari na makala ambazo wameziandika Mheshimiwa Rais ni makala ambazo zimetuleta pamoja, zimetujenga pamoja na ni makala ambazo haziligawi Taifa. Kawa kutambua mchango wa hao waandishi wa habari, Wizara imeona ni vyema nao watunukiwe zawadi na wizara,” ameeleza Prof. Kabudi.

spot_img

Latest articles

TPDC Yahimiza Wananchi Kulinda Miundombinu ya Bomba la Gesi Asilia

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuwashirikisha wananchi...

TMA yatangaza msimu wa Kipupwe Juni hadi Agosti

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kuwa na msimu...

Kamati ya Bunge yaridhishwa na uzalishaji wa kiwanda cha sukari Mkulazi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeendelea kutekeleza mikakati iliyoanishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050...

Wachina wanne wakamatwa kwa utekaji

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia raia wanne...

More like this