Jessica: Vijana jitokezeni kujiandikisha awamu ya pili ya uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Jessica Mshama ametoa wito kwa vijana wa Kitanzania nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mzunguko wa pili wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza Mei 1 hadi Julai 4, 2025.

Jessica ametoa wito huo Aprili 29, 2025 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na wito huo, Jessica ametoa onyo kali kwa watu wanaotaka kuwahadaa au kuwatumia vijana kwa misingi ya kuvuruga amani ya Tanzania.

Amesema ushiriki wa vijana katika uchaguzi ni muhimu kwa sababu kundi hilo pia lina asilimia 34.5 ya Watanzania wote kulingana na Sensa ya 2022. 

“Kila kijana mwenye umri wa miaka 18 au atakayefikisha miaka hiyo ifikapo siku ya Uchaguzi Mkuu, anatakiwa kuhakikisha amejiandikisha au ameboresha taarifa zake,” amesema.

Pia amewahimiza vijana kuchangamkia fursa za kugombea uongozi na kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu.

“Tanzania ya sasa inahitaji viongozi vijana wenye maono, uadilifu na uzalendo wa dhati,” amesisitiza.

Aidha Jessica ameeleza kuwa serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kutengeneza zaidi ya ajira milioni nane kupitia sekta za umma na binafsi, sawa na asilimia 115 ya matarajio, kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati.

Amefafanua miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Reli ya Kisasa ya SGR, Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, pamoja na ajira katika sekta za elimu na afya.

“Zaidi ya Sh. Bilioni 250 zimetolewa kwa makundi ya vijana kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi,” amesema.

Jessica pia ameeleza mafanikio mengine ya serikali ikiwemo ongezeko la upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kwa asilimia 77 na mijini kwa asilimia 88. 

Ametaja pia ujenzi wa shule mpya 3,631 za msingi na sekondari, madarasa 21,912, vituo vya afya 367 na zahanati 980.

Kwa mujibu wa Jessica, vifo vya wajawazito vimepungua kutoka 556 hadi 104 kwa kila vizazi hai 100,000 huku matumizi ya nishati safi ya kupikia yakiimarika kwa asilimia 85. Pia, huduma ya bima ya afya imeboreshwa na kuwafanya wananchi kupata matibabu kuanzia zahanati hadi hospitali za rufaa.

“Kuna watu wanabeza kwamba hakuna kulichofanyika, hawaoni haya yote yanayofanywa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Kwahiyo niwaombe vijana wenzangu msiwasikilize watu hawa kwani hawana mapenzi mema na Nchi yetu na wanataka kuvuruga amani iliyopo,” amesisitiza Jessica.

spot_img

Latest articles

TAMISA kufanya kongamano Mei 16, mwaka huu

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano...

Upanuzi wa Kituo cha Kupoza umeme Mbagala mbioni kukamilika

📌Awamu ya kwanza ya upanuzi wa Kituo Megawati 45 yakamilika 📌Asema wananchi wa Mbagala...

Rais Samia aeleza mambo ya kujifunza kutoka kwa Hayati Cleopa Msuya

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa...

TFF yamfungia miaka sita Katibu Mkuu DRFA

Na Mwandishi Wetu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),Ramadhan...

More like this

TAMISA kufanya kongamano Mei 16, mwaka huu

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano...

Upanuzi wa Kituo cha Kupoza umeme Mbagala mbioni kukamilika

📌Awamu ya kwanza ya upanuzi wa Kituo Megawati 45 yakamilika 📌Asema wananchi wa Mbagala...

Rais Samia aeleza mambo ya kujifunza kutoka kwa Hayati Cleopa Msuya

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa...