THRDC yashauri kuitishwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesema kuna umuhimu wa kukaa kwenye muafaka wa kitaifa na kukubaliana mambo ya msingi kabla ya kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktaba mwaka huu.

Mtandano huo umesema siyo afya kuona kuna mvutano unaendelea kwa sura inayoonekana na kwamba mambo yote ambayo yanalalamikiwa yanapaswa kujadiliwa kupitia mkutano wa kitaifa utakaohusisha makundi yote.

Mratibu Taifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, ameeleza hayo kufuatia mvutano unaoendelea kuhusu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye anashtakiwa kwa kosa la uhaini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

“Tunafanya kosa pale ambapo tunataka kuwazuia Watanzania wasiende kuwafuatilia ndugu zao magereza, mahakamani, hospitali na mahali popote ambapo wanahitaji kwenda kuwafuatilia…suala hili linaendelea kujenga taswira mbaya katika Serikali…nguvu kubwa inatumika pasipo sababu ya msingi,” amesema Wakili Olengurumwa.

Amesema suala hilo halipaswi kuendelea na kushauri na kwamba huu ni muda muafaka wa kuondoa changamoto zinazoendelea kwa kutumia falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan (4R) na mambo yanayolalamikiwa yanaweza yakaingia kwenye makubaliano ya muafaka na kila mmoja kwenda kwenye uchaguzi akiwa ameridhika.

“Suala hili linaweza likamalizwa kwa mazungumzo, bado tunasisitiza twende kwenye muafaka wa kitaifa kabla ya kwenda kwenye uchaguzi. Sio afya kuona mvutano unaendelea. Mambo yote ambayo yanalalamikiwa kama taifa ni nafasi ya kukaa kwenye mazungumzo na kujadiliwa, tunahitaji kuwa na mkutano wa kitaifa utakaohusisha makundi yote.

“Viongozi wa dini, siasa, serikali, polisi, tume, msajili wa vyama vya siasa, taasisi zote zinazohusika na uchaguzi wote kwa pamoja kama inawezekana tushirikiane kufanya mkutano wa kitaifa wa maridhiano…bado tunasisitiza itafutwe namna ya kutengeneza muafaka kwa taifa letu.

Wakili Olengurumwa pia amevishauri vyama vya upinzani hasa Chadema wawe tayari kwenda kwenye meza ya mazungumzo na makundi yote yashauriwe kwamba ni muhimu kushiriki na kuzingatia amani, utulivu, haki, uzalendo, umoja na upendo katika taifa.

“Yaliyotokea Kisutu tunayakemea, tunashauri vyombo vya usalama mambo ya kwenda mahakamani yanapaswa kuangaliwa kwa umakini kwa sababu suala la kwenda mahakamani ni haki ya kila Mtanzania ambaye ana ndugu na jamaa katika vyombo hivi,” amesema Wakili Olengurumwa.

spot_img

Latest articles

Msajili wa Hazina aomba ushirikiano wa PIC kuimarisha mageuzi ya uwekezaji wa umma

Na Mwandishi wetu, Dodoma OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) leo, Januari 15, 2026 imeendesha...

Serikali kupitia REA kuzindua miradi mikubwa ya kimkakati

Na Mwandishi Wetu Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatarajia kuzindua Kituo cha Kupoza...

Wachezaji Comoro waipongeza Taifa Stars

Na Mwandishi WetuBALOZI wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu leo amekutana na  wachezaji wa...

Jaji Mkuu wa Tanzania amefunua kombe

Jumatatu wiki hii Rais Samia Suluhu Hassan alifungua mkutano wa Chama cha Mahakimu na...

More like this

Msajili wa Hazina aomba ushirikiano wa PIC kuimarisha mageuzi ya uwekezaji wa umma

Na Mwandishi wetu, Dodoma OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) leo, Januari 15, 2026 imeendesha...

Serikali kupitia REA kuzindua miradi mikubwa ya kimkakati

Na Mwandishi Wetu Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatarajia kuzindua Kituo cha Kupoza...

Wachezaji Comoro waipongeza Taifa Stars

Na Mwandishi WetuBALOZI wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu leo amekutana na  wachezaji wa...