Ewura yazitaka kampuni za gesi kuongeza mawakala, kudhibiti uchakachuaji wa gesi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za nishati na Maji (Ewura) imezitaka Kampuni za gesi kuongeza idadi ya mawakala wa usambazaji kwenye maeneo mengi ili kuepusha watu kwenda kununua gesi kwa wauzaji wasio rasmi.

Wito huo umetolewa leo Aprili 24, 2025 na Meneja wa Ewura, Kanda ya Mashariki, Mhandisi Nyirabu Musira wakati akifungua semina kwa wasambazaji wa gesi za kupikia (LPG) yenye lengo la kuhakikisha usambazaji wa gesi ya LPG unafanyika kwa njia zilizo halali na salama kwa watu na mazingira.

Amesema kuwa uchakachuaji wa gesi ya kupikia ni changamoto ambayo imekuwa ikiongezeka siku za hivi karibuni ambapo wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakitumia mitungi kujaza mitungi midogo kwa kiwango hafifu.

“Zipo changamoto kadhaa kwenye biashara hii ya LPG, lakini changamoto ambayo imekuwa ikiongezeka sana kwa siku za hivi karibuni ni ujazaji haramu wa mitungi ya gesi. Licha ya kufanya hivyo ni uhalifu kisheria, lakini pia ni hatari kwa usalama wa watu na mali kwani tumeshuhudia ajali za milipuko ya mioto inayotokana na shughuli hizi.

“Niwaonye wafanyabiashara kuacha tabia hii kwani ni kinyume cha taratibu na sheria, tunaendelea na ufuatialiaji, watakaobainika hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa mawakala wa LPG kuhakikisha wanakuwa na leseni hai za Ewura na wanafanya biashara kwa kufuata masharti ya leseni.

Mhandisi Musira ameeleza kuwa matumizi ya LPG nchini yamekuwa kwa kiasi kikubwa ambapo katika kipindi cha mwaka 2023/24 kiasi cha gesi kilichoingizwa nchini ni takribani Tani za ujazo 403,638.

“Hili ni ongezeko la asilimia 38 ukilinganisha na kiasi cha Tani 293,167 zilizoingizwa nchini mwaka 2022/23. Kulingana na rekodi zetu ongezeko hili ndilo kubwa kwa takribani miaka mitano iliyopita,” amesema Mhandisi Musira.

Hata hivyo amesema kuwa, Ewura inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhamasisha matumizi sahihi ya gesi, ili kuepuka majanga ya moto yatokanayo na gesi za majumbani.

Ahmed Sharifu ambaye ni Wakala wa gesi ya Oryx Wilaya ya Temeke amesema semina hizo zinawasaidia katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku.

“Tunawashukuru Ewura kwani semina hizi zinatupa maono ya mbele na kujua matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yetu na hii inaonesha kwamba kazi kubwa ya Ewura ni kutuelimisha katika usalama na kujua utaratibu wa kupata leseni,” amesema.

spot_img

Latest articles

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...

Heche viongozi wengine Chadema waachiwa na Polisi kwa dhamana

Na Mwandishi Wetu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche na...

More like this

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...