Rais Samia aigharamia Simba safari ya Sauzi

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameiwezesha Simba  katika safari kwenda Afrika Kusini kwa kugharamia  usafiri na malazi kwa timu hiyo katika kipindi chote itakapokuwa huko kwa ajili ya mechi ya marudiano ya nusu fainali  ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch, Aprili 27, 2025.

Simba ambayo imeondoka leo, katika mchezo wa kwanza uliopigwa M kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji  amemshukuru Rais Samia  kwa sapoti hiyo, huku akisema  klabu hiyo inatambua  juhudi za Rais katika kuimarisha michezo.

“Kwa niaba ya Klabu ya Simba Sports Club, napenda kutoa shukrani za dhati kwa  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kuiwezesha klabu yetu kushiriki mashindano ya kimataifa.

“Tumepokea kwa moyo wa shukrani mchango wa malazi na usafiri kwa ajili ya mchezo wetu wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaofanyika Afrika Kusini.

spot_img

Latest articles

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this