Tume, Serikali na vyama vya siasa kusaini maadili ya uchaguzi kesho

Na Mwandishi Wetu

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, vyama vya siasa na Serikali kesho Aprili 12, 2025 wanatarajiwa kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari mkoani Dodoma leo Aprili 11, 2025 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhan amesema chama cha siasa ambacho hakitasaini maadili hayo hakitaruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Kailima amesema maadili hayo yameandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha 162 (1), (2) na (3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 ambacho kinaitaka Tume baada ya kushauriana na vyama vyote vya siasa na Serikali, kuandaa na kuchapisha katika Gazeti la Serikali Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zitakazoainisha maadili ya vyama vya siasa, Serikali na Tume wakati wa kampeni za uchaguzi na uchaguzi na utaratibu wa utekelezaji wake.

Amesema kifungu hicho kinaelekeza kuwa kanuni za maadili zitasainiwa na kila chama cha siasa, kila mgombea kabla hajawasilisha fomu ya uteuzi, Serikali na Tume zitapaswa kuzingatia na wahusika wote waliosaini.

Ameongeza kuwa tayari maandalizi yote muhimu yameshafanyika na mawasiliano yameshafanyika baina ya Tume, Serikali na vyama vya siasa na kwamba kinachosubiriwa ni kuwasili kwa wahusika jijini Dodoma kwa ajili ya kusaini kanuni hizo za maadili kesho.

Amefafanua kuwa zoezi hilo litafanyika kwa siku moja tu na kwamba baada ya hapo chama ambacho hakijasaini kanuni hizo za maadili hakitapata fursa ya kusimamisha wagombea.

Katika hatua nyingine, Kailima amesema Tume inaendelea vizuri na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba tayari imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura huku maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwa awamu ya pili yanaendelea ambapo Tume inatarajiwa kutangaza ratiba ya zoezi hilo hivi karibuni.

Kifungu cha 16(5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, ambacho kinaipa Tume jukumu la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili, kati ya uchaguzi mkuu mmoja uliomalizika na siku moja kabla ya uteuzi wa wagombea wa uchaguzi mkuu unaofuatia.

Tayari Tume imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari ambao ulifanyika nchi nzima kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 hadi tarehe 25 Machi, 2025.

spot_img

Latest articles

Waogeleaji wa Lake Victoria Sports Club waahidi kuing’arisha Tanzania Kimataifa

Na Mwandishi Wetu Jumla ya waogeleaji sita  chipukizi wa Lake Victoria Sports Club  ya jijini...

Mbunge Kimei kinara kuzungumzia mahitaji ya wananchi

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei ametajwa kuwa...

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...

Kafulila: Hatuwezi kujenga uchumi wa nchi bila kushirikisha sekta binafsi

Na Tatu Mohamed, Mwanza MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma...

More like this

Waogeleaji wa Lake Victoria Sports Club waahidi kuing’arisha Tanzania Kimataifa

Na Mwandishi Wetu Jumla ya waogeleaji sita  chipukizi wa Lake Victoria Sports Club  ya jijini...

Mbunge Kimei kinara kuzungumzia mahitaji ya wananchi

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei ametajwa kuwa...

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...