Rais Samia afanya mazungumzo na Mmiliki wa Klabu ya Manchester United, Ratcliffe

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Aprili 11, 2025.

Katika mazungumzo yao Rais Dkt. Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibiti muingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Kupitia Taasisi yake ya Six Rivers, Sir Jim Ratcliffe amebainisha kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhi ya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo.

spot_img

Latest articles

Makamu wa Rais atangaza kujiuzulu

Makamu wa Rais wa Tanzania, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kuanzia...

RAIS SAMIA AAGIZA WAKUU WA MIKOA KUJIANDAA NA UDHIBITI WA ATHARI ZA ELNINO

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Rais Samia azindua Kituo cha kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

JNHPP kuongeza Umeme wa Gridi ya Taifa kwa asilimia 45

Na Tatu Mohamed BWAWA la Julius Nyerere (JNHPP) linatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo...

More like this