Usafiri Dar kwenda Mikoa ya Kusini warejea

Na Mwandishi Wetu

USAFIRI umeanza kurejea katika barabara kuu kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi baada ya wataalamu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya kazi usiku na mchana kurekebisha eneo la Somanga Matandu lililoharibiwa na mvua na kufanya njia isipitike.

Daraja la Somanga lilikatika Aprili 06, 2025 huku lile la Mto Matandu likikatika Aprili 07, 2025 na kusababisha adha kwa abiria wanaotumia Barabara hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ambaye ameweka kambi katika eneo hilo tangu jana, amewaambia waandishi wa habari kuwa magari madogo 230, mabasi 10 na baadhi ya malori 30 yaliyobeba bidhaa mbalimbali yakiwemo mawe makubwa yamefanikiwa kupita katika eneo la Somanga Mtama na Matandu leo kati ya saa 11:30 alfajiri hadi saa 12:00 asubuhi.

Ulega ameyasema hayo leo Aprili 8, 2025 wakati akitoa taarifa ya awali akiwa mkoani Lindi wakati akiendelea kusimamia zoezi la urejeshaji wa maeneo yaliyokatika katika barabara kuu ya Dar es Salaam – Lindi linaoofanywa na wataalamu wa Wizara ya Ujenzi na TANROADS kwa kushirikiana na mkandarasi.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

More like this