Dkt. Biteko ashiriki uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Pwani

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo Aprili 2, 2025 Kibaha mkoani Pwani katika viwanja vya Shirika la Elimu ameshiriki katika sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani humo.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango.

Sherehe hizo zilizoongozwa na kauli mbiu: ‘Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu’ zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Viongozi wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

spot_img

Latest articles

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...

Yanga yatua Zanzibar kuitengenezea dozi AS FAR Rabat

Na Winfrida Mtoi Kikosi cha Yanga kimetua visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya kuikabili AS FAR...

Rais Samia atangaza Baraza Jipya la Mawaziri, nane watemwa

Tatu Mohamed na Winfrida Mtoi RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,...

More like this