SIMBA YAIFUATA AL MASRY NA HESABU KALI

Na Winfrida Mtoi

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka Machi 28,2025 kuifuata timu ya Al Masry nchini Misri kwa mchezo wao wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika huku uongozi wa klabu hiyo ukiwa na hesabu za kutinga nusu fainali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Habari na Mawasiliano wa hiyo, Ahmed Ally amesema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanavuka hatua ya robo fainali na kutinga nusu fainali.

Ahmed amesema licha ya kukutana na mpinzani mgumu hatua ya robo fainali lakini wamejipanga kuhakikisha wanavuka na ndiyo sababu ya kuja na kauli mbiu ya ‘Hii tunavuka’.

“Kwa miaka mitano mfululizo tumekuwa tukiishia robo fainali kwenye michuano ya Afrika lakini safari hii tumedhamiria kuhakikisha tunavuka,”amesema Ahmed.

Aidha amesema wachezaji waliokuwa sehemu ya timu ya taifa, Taifa Stars, wataungana na wenzao nchini Misri ili kukamilisha maandalizi ya mchezo huo wakati Camara na Mukwala, tayari wamewasili na kuungana na wenzao kwa maandalizi zaidi kabla ya safari.

spot_img

Latest articles

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

Makocha Yanga, Simba waanika kinachowapa jeuri

Na Winfrida Mtoi Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kesho Septemba 16,2025, makocha wa Simba...

CAF yaipiga faini Simba, kucheza bila mashabiki

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba imepigwa faini ya Dola za Marekani 50,000 (...

More like this

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

Makocha Yanga, Simba waanika kinachowapa jeuri

Na Winfrida Mtoi Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kesho Septemba 16,2025, makocha wa Simba...