NACTVET yawahakikishia wadau usimamizi thabiti wa ubora wa elimu ya Ufundi na Amali

Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limeelezea dhamira yake kuhakikisha kuwa mafunzo ya ufundi na yale ya amali yanayotolewa kwenye vyuo na shule za sekondari za ufundi nchini yanazingatia viwango na ubora ili kuzalisha wahitimu wanaokubalika katika soko la ajira.

Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwajuma Lingwanda, ameeleza hayo Machi 19, 2025, wakati akichangia mada kuhusu mchango wa wahitimu wa ufundi stadi katika maendeleo ya jamii na uchumi, kwenye kongamano la maadhimisho ya miaka 30 ya VETA, linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mwajuma amesema matarajio ya Serikali ni kuwa na wahitimu wa ufundi na amali watakaochangia kikamilifu katika shughuli za uzalishaji kupitia ujuzi walioupata.

Amesisitiza umuhimu wa kufanyika tafiti za mara kwa mara katika sekta ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, ili kuwezesha uandaaji wa mikakati madhubuti ya kuboresha utoaji mafunzo kulingana na mahitaji ya viwanda na soko la ajira kwa ujumla.

“Tafiti za mara kwa mara zitasaidia kutoa taarifa sahihi kuhusu mahitaji ya soko la ajira na kutoa mrejesho kuhusu wahitimu wa ufundi, hivyo kuboresha utoaji mafunzo kwenye vyuo vyetu,” amesema Dkt. Mwajuma.

Amewahakikishia wadau kuwa NACTVET itaendelea kushirikiana nao katika kuimarisha utoaji mafunzo ya ufundi na kuzalisha wahitimu wenye sifa watakaoweza kuajirika na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

Aidha amesema NACTVET inatarajia kuja na mfumo maalum wa kieletroniki utakaochakata takwimu na taarifa mbalimbali zinazotoka katika Vyuo vya Ufundi na Ufundi Stadi,Wahitimu,Waajili na wale wanaojiajili.

Amesema awali walikuwa wakitumia njia ya kawaida katika kukusanya takwimu na taarifa hizo hivyo baada ya mfumo huo utaweza kuwarahisishia kazi yao kwa urahisi na ufanisi.

“Sasa hivi tunataka kutengeneza mfumo utakaokuwa unakusanya taarifa kutoka kwa wahitimu wa taasisi za ufundi na Ufundi stadi kwa njia rahisi zaidi. Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia bajeti ya nyongeza mwaka huu.

“Jukumu letu kama baraza ni kuhakikisha tunakuwa na taarifa au takwimu ambazo ni sawa ambazo zitaweza kufanyiwa kazi na watafiti pindi wanataka kujua mambo mbalimbali ya wahitimu ikiwemo walioajiriwa au waliojiajiri wapo wangapi hadi sasa,” amesema.

spot_img

Latest articles

Chalamila awaalika wakazi wa Dar kujitokeza kwa wingi uzinduzi wa Kituo cha biashara cha EACLC

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaalika Watanzania na...

Ajali ya moto yaua watoto yatima watano

Na Mwandishi Wetu Watoto watano waliokuwa wanalelewa katika kituo cha watoto yatima cha Igambilo Manispaa...

Januari Makamba hayumo, Nape apeta uteuzi CCM

Na Mwandishi wetu Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Rais wa Yanga akatwa uteuzi Jimbo la Kigamboni, Jemedali, Shafii Dauda mambo mazuri

Na Mwandishi Wetu Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Saidi ameshindwa kupenya katika  uteuzi...

More like this

Chalamila awaalika wakazi wa Dar kujitokeza kwa wingi uzinduzi wa Kituo cha biashara cha EACLC

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaalika Watanzania na...

Ajali ya moto yaua watoto yatima watano

Na Mwandishi Wetu Watoto watano waliokuwa wanalelewa katika kituo cha watoto yatima cha Igambilo Manispaa...

Januari Makamba hayumo, Nape apeta uteuzi CCM

Na Mwandishi wetu Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)...