UPOTEVU WA MAJI WASABABISA HASARA YA SH 114.12 BILIONI

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amezielekeza mamlaka za maji kupunguza kiwango cha upotevu maji ili kuepusha hasara ya sh 114.12 bilioni  iliyotokana na upotevu huo kwa mwaka huu.

Dk. Biteko amesema hayo jijini Dar es Salaam Machi 19, 2025 wakati akizindua  taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za maji kwa mwaka 2023/24 na kusema upatikanaji wa huduma za maji ni haki ya msingi hivyo ni muhimu kulinda vyanzo vya maji kuwezesha upatikanaji wake.

Amesema pamoja na jitihada zinazoendelea jamii ina wajibu wa kuhakikisha usafi wa mazingira, kupanda miti na kuhifadi misitu ili kuendelea kupata na kutumia rasilimali maji.

“Tusipotunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira tutajikuta katika mtanziko mkubwa (water Stress),” amesema na kuongeza kuwa kukosekana kwa rasilimali maji kwa baadhi ya watu kinaweza kuwa chanzo cha migogoro na machafuko katika jamii husika.

Amesema hadi sasa asilimia 84 kwa mijini na asilimia 79.6 kwa maeneo ya vijijini zimeunganishwa na huduma ya maji ambapo kuna ongezeko la asilimia 7 kutoka kipindi cha mwaka uliotangulia.

Awali, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kumekuwa na ongezeko la ubora wa viwango vya maji na udhibiti wa upotevu wa maji ambao unasababisha hasara kubwa hasa unapothamanishwa kifedha.

Hata hivyo ameipongeza EWURA kwa kazi nzuri na kutoa taarifa inayoonesha uhalisia wa mambo huku akisema mamlaka zinazofanya vizuri zinapata tuzo ikiwa ni motisha ya ushindani wa kimaendeleo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Mark Mwandosya ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele na kuongeza bajeti ambayo imeongezeka kutoka sh 206 bilioni  mwaka 2010/11 hadi sh 558 bilioni  mwaka 2024/25

Amesema uwekezaji wa katika sekta ya maji unaleta faida zaidi ya mara saba ya mtaji ambapo uwekezaji wa dola 1 unaweza kuleta faida ya dola 7 katika uchumi wa taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dk. James Andelile amesema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa bado kuna changamoto kadhaa zinazotokana na utegemezi wa Mamlaka za maji kwa Serikali.

Pia amesema changamoto nyingine ni uchakavu wa miundombinu ya maji inayosababisha upotevu wa maji na hasara kwa serikali.

Mamlaka za maji zilizofanya vizuri katika udhibiti wa upotevu wa maji na asilimia ya maji yanayopotea ni Maganzo 4%, Nzega 6%, Kashuwasa 11%, Biharamulo 12% na Mwanuzi 13%.

Mamlaka zilizoshindwa kudhibiti upotevu huo kwa kiwango kikubwa ni Rombo 70%, Handeni 69%, Mugango/kyabakari 68%, Ifakara 56% na Kilindoni 55%.

spot_img

Latest articles

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...

CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la...

More like this

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...