Mchengerwa amtaka mkandarasi wa Daraja la Mbambe kuongeza kasi ya ujenzi

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala, Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya Nyanza Road Works kuongeza kasi ya ujenzi wa Daraja la Mbambe lenye urefu wa mita 81 ili likamilike kwa wakati na kuondoa adha inayowakabili wananchi wa Wilaya ya Rufiji.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kijiji cha Mbambe ya kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.

“Mkandarasi ongeza kasi ya ujenzi wa daraja hili kwani asilimia 22 iliyofikiwa bado ni ndogo sana. Kwa mwendo huu, mvua zikiongezeka zitaleta changamoto itakayokwamisha ujenzi,” amesema.

Aidha, amewataka wananchi wa Kijiji cha Mbambe kushirikiana na uongozi wa wilaya kwa kutoa taarifa pale wanapoona hali ya kusuasua katika ujenzi wa daraja hilo na kuwahakikishia kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ametoa fedha kwa ajili ya fidia kwa wote waliopitiwa na mradi huo, ambao unahusisha pia ujenzi wa barabara za maingilio zenye urefu wa kilomita 3.

“Mkuu wa Wilaya, naelekeza Meneja wa TANROADS wa mkoa kuhakikisha kuanzia wiki ijayo fidia inalipwa kwa wale wote waliokwishahakikiwa madai yao. Rais Samia ameshatoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya fidia,” ameagiza Mchengerwa.

Hata hivyo, Waziri Mchengerwa amewataka wananchi wa Mbambe na Rufiji kwa ujumla kupuuza taarifa potofu kwamba mradi wa daraja hilo umesimama, akisisitiza kuwa ujenzi unaendelea.

Awali, Msimamizi wa Mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works, Mhandisi Emmanurel Owoya, amesema kuwa ujenzi huo umefikia asilimia 22, ambapo tayari nguzo za msingi 64 kati ya 107 zimejengwa na Sh.Bilioni 24.16 zitatumika kukamilisha ujenzi wa Daraja la Mbambe, likijumuisha barabara za maingilio za kilomita 3 kwa pande zote mbili za daraja.

spot_img

Latest articles

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Tanesco akabidhiwa rasmi ofisi

📌Asema TANESCO imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme 📌Apongeza jitihada zinazoendelea za...

Sowah, Kante wafungiwa, Aucho naye yumo

Na Winfrida Mtoi NYOTA wa Simba Jonathan Sowah na Allasane Kante wamefungiwa michezo mitano na...

Dk. Mwigulu: Tutamuenzi kwa vitendo marehemu Jenista

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itayaendeleza mambo yote mema yaliyofanywa na...

Balozi Bandora kuzikwa kesho makaburi ya Kinondoni

Mwanadiplomasia nguli wa Tanzania, aliyewahi  kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mratibu Mkazi...

More like this

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Tanesco akabidhiwa rasmi ofisi

📌Asema TANESCO imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme 📌Apongeza jitihada zinazoendelea za...

Sowah, Kante wafungiwa, Aucho naye yumo

Na Winfrida Mtoi NYOTA wa Simba Jonathan Sowah na Allasane Kante wamefungiwa michezo mitano na...

Dk. Mwigulu: Tutamuenzi kwa vitendo marehemu Jenista

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itayaendeleza mambo yote mema yaliyofanywa na...