Na Mwandishi Wetu
JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itatuma ujumbe nchini Angola siku ya Jumanne kwa ajili ya mazungumzo yenye lengo la kusuluhisha mzozo unaoendelea dhidi ya waasi wanaaminika kuungwa mkono na Rwanda Mashariki, ofisi ya Rais ilisema Jumapili.
Angola ilisema wiki iliyopita kuwa mazungumzo ya moja kwa moja ya amani kati ya DRC na waasi wa M23 yataanza katika mji mkuu wa Angola Luanda mnamo Machi 18.
Rais Felix Tshisekedi, ambaye kwa muda mrefu amefutilia mbali mazungumzo na M23, alikuwa akifikiria kubadili msimamo wake baada ya uungwaji mkono wa kikanda kwa Kongo ukipungua.
“Kwa wakati huu, hatuwezi kusema ni nani atakayekuwa sehemu ya ujumbe,” msemaji wa ofisi ya rais Tina Salama alisema.

M23 imekubali kupokea mwaliko wa Angola, msemaji wake Lawrence Kanyuka alisema siku ya Jumapili, bila kusema kama itashiriki.
M23 ilitoa madai kadhaa baada ya mazungumzo hayo kutangazwa, ikiwa ni pamoja na kumtaka Tshisekedi aeleze hadharani dhamira yake ya kujadiliana nao moja kwa moja.