Lukuvi aitaka Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuweka mifumo rafiki ya usambazaji nyaraka kwa Wananchi

Na Mwandishi Wetu

IDARA Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali yatakiwa kuweka mifumo mizuri ya usambazaji wa nyaraka za wazi kwa wananchi kupitia mifumo ya kidigitali na hata kwa mifumo ya nyaraka ngumu ili wananchi wanufaike na taarifa hizo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi alipofanya ziara katika Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kujionea maendeleo ya ujenzi na ufungaji wa mitambo mipya ya uchapishaji wa nyaraka za serikali.

Amesema, nyaraka nyingi na muhimu huchapwa kwenye Gazeti la Serikali hivyo mkiongeza uelewa kwa wananchi juu ya namna ya kulipata Gazeti la Serikali inarahisha taarifa hizo muhimu kufikia walengwa.

“Tunaweza kufanya jitihada hizi za kusambaza taarifa la Gazeti la Serikali kupatikana katika shule kwa njia za kidigitali kupita mifumo ya computa ambazo zimeanza kutumika katika utoaji wa elimu ili wanafunzi waweze kuzipata,” alifafanua

Nitoe rai kwa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali hasa kwenye nyaraka ambazo ni za wazi fanyeni uelimishaji ili taarifa Magazeti ya Serikali ziweze kuwafikia wananchi.

“Tunaamini Serikali kwa kununua mitambo hii ya kisasa itasaidia Watendaji wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kujiweka sawa kimafunzo na maadili ili utunzaji wa nyaraka na siri uzidi kuimarika,” alisisitiza.

Hivyo basi Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali inaendelea kuwa mhimili Mkuu wa Serikali kwa miaka yote katika uchapishaji wa nyaraka za Serikali hasa zinapokuwa nyaraka nyingi na nyeti na zinahitajika kwa uharaka.

Kwa upande wake Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali George Lugome amesema wanatengeneza mfumo wa mtandao ambao utamsaidia mteja kujaza taarifa zake na kufanya malipo kwa njia ya mtandao na tangazo kutoka katika gazeti la serikali.

Ameongeza kusema: “mfumo wa mtandao hauhusiki taarifa za mirathi ambazo uwasilishaji wake unahitaji Mhusika kuleta vielelezo vyake vya uthibitisho kwa mujibu sheria,”.

Mpiga Mchapa amesema, kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika ununuaji wa mashine za kisasa utasaidia katika kuongeza uzalishaji na kuongeza maduhuli ya Serikali.

spot_img

Latest articles

Taifa gas yatangaza kutokupandisha bei ya gesi ya majumbani

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taifa Gas imetangaza kuwa haitapandisha bei ya gesi ya majumbani...

Bosi wa mafuta atumbuliwa

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti...

Nishati Safi yafungua milango ya fursa kwa watengeneza maudhui

Na Mwandishi Wetu, Mwanza WATENGENEZA maudhui nchini wamehamasishwa kutumia ubunifu wao kujipatia kipato kupitia fursa...

WARAKA WA MWANDOSYA KUMBUKUMBU YA MWAPACHU

KUMKUMBUKA MAREHEMU BALOZI JUMA VOLTER MWAPACHU Balozi Juma Volter Mwapachu (Mwenyezi Mungu Amrehemu), mwanasheria, mwanadiplomasia,...

More like this

Taifa gas yatangaza kutokupandisha bei ya gesi ya majumbani

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taifa Gas imetangaza kuwa haitapandisha bei ya gesi ya majumbani...

Bosi wa mafuta atumbuliwa

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti...

Nishati Safi yafungua milango ya fursa kwa watengeneza maudhui

Na Mwandishi Wetu, Mwanza WATENGENEZA maudhui nchini wamehamasishwa kutumia ubunifu wao kujipatia kipato kupitia fursa...