Mramba: Kununua umeme nje ya nchi, haimaanishi kuna upungufu nchini

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa ununuzi wa Umeme kutoka nchi Jirani haimaanishi kuwa nchi iko katika changamoto ya upungufu wa umeme kwa kuwa mpaka sasa Tanzania inazalisha umeme wa kutosha ambao ni takribani Megawati 3796.

Aidha amesema kuwa kununua na kuuziana umeme kwa nchi si jambo geni na Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikinunua umeme nchini Uganda kwa ajili ya Mkoa wa Kagera, nchini Zambia kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa na nchini Kenya kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tanga hususani ya mpakani.

Ameyasema hayo leo Machi 10, 2025 wakati akitoa Ufafanuzi zaidi kuhusu hatua ya Serikali kununua Umeme nchini Ethiopitia kupitia Nchini Kenya hadi Namanga Mkoani Arusha utaimarisha Upatikanaji wa Umeme katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambayo kimsingi kwa sasa inatumia umeme unaozalishwa katika Mikoa ya Kusini.

Amefafanua kuwa hatua hii ina faida kwa pande zote mbili kwa kuwa njia itakayotumiwa kununua umeme nchini Ethiopia ndio hiyo itakayotumiwa kuuza umeme kwa nchi zenye Uhitaji.

Akifafanunua zaidi amesema kuwa jinsi umeme utakavyokuwa ukinunuliwa, umeme wa Ethiopia utaingizwa kwenye mfumo wa Gridi ya Kenya na kisha Kenya itatoa umeme kuja Tanzania ikifidia umeme ulioingizwa kutoka nchini Ethiopia.

“Uamuzi wa Tanzania kuchukua umeme Ethiopia ni kitu chenye faida na sio hasara kama watu wanavyodhani, kwani baadhi ya vyanzo vya umeme hapa nchini vinazalisha uniti moja kwa bei kubwa kuliko bei ambayo umeme huo utanunuliwa kutoka Ethiopia.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa ridhaa kuruhusu umeme kuingia Kaskazini kutoka nchi Jirani kutokana na hali ya umeme kanda ya Kaskazini kuwa inaingia kidogo katika gridi ya Taifa katika kanda hii,” amesema.

Ameongeza kuwa, tayari kuna nchi zimekuja zinataka kununua umeme nchini ambapo kama nchi inaweza kuwauzia kwa bei kubwa kuliko unaonunuliwa Ethiopia.

Amesema umeme huo unaotoka nchini Ethiopia utasaidia kwa kiasi kikubwa umeme kuimarika kwa kanda ya Kaskazini kwani hali ya umeme kutokuwa na nguvu kumalizika.

“Umeme unaopelekwa mikoa ya Kaskazini unapotea kwa kiwango cha megawati 17 ambazo zinatosha kuhudumia Mkoa wa Songwe ambao unatumia megawati 14, hivyo tukisema tuutoe Bwawa la Mwalimu Nyerere kunakuwa na upotevu wa umeme mwingi.

spot_img

Latest articles

Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa...

2025 mwaka wa mageuzi na matokeo katika mashirika ya umma

Na Mwandishi Wetu MWAKA 2025 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Ofisi ya Msajili wa...

Wakatoliki feki wamechafua hali ya hewa, aibu hii anabeba nani?

TAHARUKI kubwa imeibuka nchini. Unaweza kuiona ukichungulia kwenye mitandao ya kijamii. Imesababishwa na akili...

Mukwala atua Zanzibar, Simba ikiivaa Azam kesho Mapinduzi Cup

Na Winfrida Mtoi WAKATI Simba kitarajia kukabiliana na Azam FC kesho katika mchezo wa nusu...

More like this

Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa...

2025 mwaka wa mageuzi na matokeo katika mashirika ya umma

Na Mwandishi Wetu MWAKA 2025 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Ofisi ya Msajili wa...

Wakatoliki feki wamechafua hali ya hewa, aibu hii anabeba nani?

TAHARUKI kubwa imeibuka nchini. Unaweza kuiona ukichungulia kwenye mitandao ya kijamii. Imesababishwa na akili...