Kamishna Shirima: Tutaendelea kutengeneza sera rafiki kuvutia Uwekezaji sekta ya mafuta na gesi asilia

Na Mwandishi Wetu

KAMISHNA wa Petroli, Goodluck Shirima amesema kuwa, Tanzania imejipanga vyema kutengeneza sera rafiki zitakazozidi kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya Mafuta na Gesi Asilia ambazo zitawezesha pia kupata mitaji ya kuendesha Sekta kwa ufanisi.

Kamishna Shirima amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25) linalofanyika kwa Siku Tatu jijini Dar es Salaam.

“Katika Mkutano wa EAPCE’25 tumejadili kuhusu umuhimu wa kuwa na mikataba ambayo ina uwazi, inayotabirika na yenye manufaa kwa nchi na kwa wawekezaji. Mabenki na taasisi za kifedha zipo tayari na zina hamu ya kufadhili miradi hii, sisi kama Serikali jukumu letu ni kutengeneza mazingira sahihi kupitia sera zetu na sheria,” amesema.

Kuhusu Sekta ya Mafuta nchini, amesema kuwa imeimarika kwani mafuta yapo na yanapatikana kwa bei himilivu na kwamba sasa bei ya kushushia mafuta kwenye bandari zote zinafanana kwa lengo la kupunguza gharama kwa Watanzania.

Kuhusu Mkondo wa kati wa petroli, Shirima amesema kuwa Serikali inaendelea kuwa na miradi ya kimkakati ya usafirishaji mafuta na gesi ambapo Serikali ya Tanzania na Zambia ziko kwenye mazungumzo ili kujenga bomba jipya la kusafirisha mafuta ambalo litasaidia kusambaza mafuta pia katika sehemu ambazo linapita kama vile Morogoro, Njombe na Mbeya.

Ameongeza kuwa, kuna mazungumzo yanaendelea na Serikali ya Uganda ili kujenga bomba la kusafirisha mafuta safi kutoka Tanzania kwenda Uganda na pia ujenzi wa bomba la gesi kwenda nchini humo ambalo pia litasambaza gesi sehemu ambazo linapita.

Amesema kuwa chini ya uongozi madhubuti wa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko miradi hiyo itatekelezwa kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Mhandisi Joyce Kisamo kutoka Wizara ya Nishati amesema kuwa mkutano huo ambao umeendeshwa kwa mafanikio umehudhuriwa na Viongozi wa Ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Mawaziri, Makatibu pamoja na Wataalam wabobezi wa Sekta kutoka nchi 6 za Afrika Mashariki.

spot_img

Latest articles

NEMC yatoa elimu kwa umma kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri

Na Tatu Mohamed BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeanza kutoa...

Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua...

Naibu Waziri wa Nishati akabidhi vitendea kazi Kwa Tanesco Mkoa wa Shinyanga

📌Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi 📌Awasihi wananchi kutumia...

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....

More like this

NEMC yatoa elimu kwa umma kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri

Na Tatu Mohamed BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeanza kutoa...

Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua...

Naibu Waziri wa Nishati akabidhi vitendea kazi Kwa Tanesco Mkoa wa Shinyanga

📌Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi 📌Awasihi wananchi kutumia...