Watumishi Tume ya Madini wajengewa uwezo matumizi ya mashine za kupima madini ya metali

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo amewataka watumishi wa Tume kufanya kazi kwa kujituma na weledi hasa kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini ili Sekta ya Madini iendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa.

Mhandisi Lwamo ametoa rai hiyo, leo Februari 25, 2025 jijini Dodoma akifungua mafunzo ya matumizi ya mashine maalum za kupima madini ya metali kwa njia ya Mionzi /X-RAY kwa watalam wa Tume ya Madini wakiwemo Wahandisi Migodi, Wahasibu, Watakwimu, Maafisa Utawala na Wataalam wa Maabara ‘Lab Technologist.

Amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa Tume ya Madini rekodi ya makusanyo ya maduhuli ya Serikali imeendelea kukua hali iliyopelekea wadau wengi wa madini na wananchi kwa ujumla kuwa na taswira chanya ya Tume.

“Mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 tulimaliza kwa kukusanya Shilingi Bilioni 753, mwaka huu tunatakiwa kukusanya Shilingi Trilioni Moja, sote tunapaswa kuwa na weledi ili tuweze kufikia lengo, hatuwezi kufika bila uadilifu, kujituma na kutunza vitendea kazi,” amesema Mhandisi Lwamo.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Lwamo amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini itaendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, Masoko ya Madini, Vituo vya Ununuzi wa Madini na Maabara ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini nchini.

Naye Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Venance Kasiki amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha watumishi wanajengewa uwezo wa matumizi sahihi ya mashine za kupima madini ya metali ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia sana kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.

spot_img

Latest articles

Dk. Mwigulu ajadiliana na Kamati ya Maandalizi AFCON 2027

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi...

Coastal Union yawatembezea kichapo maafande wa Magereza

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Coastal Union imetembeza kichapo cha mabao 4-1 kwa maafande wa...

Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna...

Msajili wa Hazina aikaribisha Jeune Afrique Media Group kuangazia fursa za uwekezaji

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Frederic...

More like this

Dk. Mwigulu ajadiliana na Kamati ya Maandalizi AFCON 2027

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi...

Coastal Union yawatembezea kichapo maafande wa Magereza

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Coastal Union imetembeza kichapo cha mabao 4-1 kwa maafande wa...

Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna...