Serikali, wadau waombwa kusapoti mashindano ya Lina PG Tour

Na Mwandishi wetu

SERIKALI wakiwemo wadau mbalimbali wa michezo hasa wa gofu wameombwa kusapoti mashindano ya Lina PG Tour yanayofanyika kila mwaka kwa lengo la kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake marehemu Lina Nkya.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na familia ya Said Nkya kwa kushirikiana na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) yanaingia msimu wa pili kwa mwaka huu na yanatarajia kuanza kutimua vumbi Februari 27 hadi Machi 2, 2025 mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa waandaaji na kiongozi wa mashindano hayo, Ayne Magombe amesema wanaiomba serikali na wadau kujitokeza kwa wingi kusapoti mashindano hayo yenye lengo la kuendelea kukuza mchezo huo na kupata wachezaji wengi watakaoiwakilisha Tanzania kimataifa.

Amesema kuendesha mashindano ni gharama hivyo kupitia wadau mbalimbali na serikali kwa ujumla wakijitokeza na kuwapa sapoti wataweza kuendelea kufanya mashindano hayo kila mwaka na kupata zawadi nyingi zaidi za kuwapatia washindi.

“Tunawaomba wadau wajitokeze kutusapoti kwani ni gharama kubwa kuendesha mashindano haya, tunapokuwa na watu wengi zaidi wa kutishika mkono itatusaidia kukuza mchezo huu na kupata wachezaji wengi watakaokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa,” amesema Magombe.

Hata hivyo Magombe amesema wazo la kuanzisha mashindano hayo lilitoka kwa mama mwenyewe Lina ambaye alikuwa akiupenda mchezo huo hasa kwa kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kucheza.

“Hivyo familia nayo ikaona ni vema kuendeleza wazo hilo kwa kuanzisha mashindano haya ambayo yamekuwa chachu kwa wachezaji wengi wa gofu kushiriki,” amesema Magombe.

Kuhusu mashindano, Magombe amesema msimu wa pili utaanza rasmi Februari 27 hadi Machi 2, 2025 katika viwanja vya gofu Gymkhana Morogoro hivyo amewataka wachezaji kujitokeza kwa wingi kushiriki.

Kwa upande wake Mchezaji wa kulipwa wa gofu kutoka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Hassan Kadio amesema shindano hilo la Lina Pg Tour ni la kipekee kwani ndilo linalotoa zawadi kubwa kwa sasa ambazo zinahamasisha watu wengi kujitokeza kushiriki.

“Nawaomba wadau wajitokeze kwa wingi kuisapoti Lina PG Tour, kwangu mimi tangu nianze kucheza gofu ndilo shindano pekee Tanzania ambalo limekuwa ni tour na linalotoa zawadi kubwa ambazo zinawahamasisha watu kwenda kushiriki hivyo niwaombe wadau waje kuisaidia Lina Tour,” amesema Kadio.

Naye mchezaji wa gofu wa kulipwa kutoka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Fadhil Nkya amesema ni muhimu wadau kujitokeza kusaidia Lina Tour ambayo imejikita kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji mbalimbali.

“Kwa miaka mitano ijayo naiona gofu mbali sana, wadau wakijitokeza kutusaidia tunaweza kufanya makubwa, tumeanza mwaka jana lakini matokeo mazuri yamejitokeza, tunawaomba watu watushike mkono na wachezaji waendelee kujitokeza kushiriki huu mchezo,” amesema.

Lina Nkya anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika mchezo huo na urithi wake umejengwa kupitia ufanisi wa kipekee, juhudi zisizo na kifani, na mapenzi kwa gofu ambayo yamehamasisha vizazi vingi.

spot_img

Latest articles

Ndejembi: Ufanisi wa Tanesco katika utekelezaji na Usimamizi wa miradi umeleta mfumo madhubuti wa Nishati

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme...

Maboresho ya mitambo ya kufua umeme Mtera yaimarisha uzalishaji umeme

Na Mwandishi Wetu, Mtera NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Novemba 26, 2025, alitembelea na...

Ndejembi: Tanzania sasa ina umeme wa kutosha

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Tanzania kwa sasa ina umeme...

Jeshi la Polisi lachunguza  taarifa ya OCD  Chunya

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi limesema limeona na linafanyia uchunguzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao...

More like this

Ndejembi: Ufanisi wa Tanesco katika utekelezaji na Usimamizi wa miradi umeleta mfumo madhubuti wa Nishati

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme...

Maboresho ya mitambo ya kufua umeme Mtera yaimarisha uzalishaji umeme

Na Mwandishi Wetu, Mtera NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Novemba 26, 2025, alitembelea na...

Ndejembi: Tanzania sasa ina umeme wa kutosha

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Tanzania kwa sasa ina umeme...