Na Mwandishi Wetu
Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Equatorial Guinea katika mchezo wa kufuzu WAFCON 2026 uliochezwa leo Februari 20, 2025 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na Stumai Abdalah dk 49, Enekia Kasongo dk 55 na Diana Lucas dk 90+, huku bao la Equatorial Guinea likifungwa na Getrudis Engueme dk 42.
