Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Singida Black Stars imemshauri aliyekuwa kocha wa timu hiyo Patrick Aussems kuanzisha timu kama anaguswa na Soka la Tanzania ili afanye yale anayoshari kwa vitendo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Februari 19,2025,imejibu kauli ambazo kocha huyo amekuwa akizitoa ikiwamo sababu za kufukuzwa kwake kwenye klabu hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa Aussems aliondolewa kutokana na matokeo mabaya ya michezo mitatu ikiwamo pia kukosa sifa ya kuwa kocha mkuu kulingana na elimu yake.


