Waziri Mkuu akutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2025 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Christine Grau, Ofisini ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania itaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na nchi za Umoja wa Ulaya.

“Inatia faraja sana kuona kuna ukuaji wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya, Umoja wa Ulaya umewekeza takriban euro bilioni tatu nchini, hii kwa kiasi kikubwa imechangia kutengeneza ajira na makusanyo ya kodi,” amesema.

Ameongeza kuwa, Tanzania itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuzivutia sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Pia, Majaliwa amesema kuwa Tanzania inathamini msaada mkubwa ambao unatolewa na Umoja wa Ulaya katika kuchangia shughuli za maendeleo nchini.

“Katika kipindi cha 2021-2027, Umoja wa Ulaya umetenga euro milioni 703 ili kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, tunakushukuru hasa kwa kujitolea kwenu kuimarisha ushirikiano huu,” amesema Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa amekutana pia na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Ahn-Eun-Ju ambaye alimweleza kuwa Tanzania inajivunia ushirikiano na nchi hiyo kwenye sekta mbalimbali za maendeleo na Jamhuri ya Korea zinaushirikiano mkubwa wa kibiashara kwa miaka mingi, mnamo mwaka 2023, kiwango cha ufanyajibiashara kilifikia dola milioni 672.7, ikilinganishwa na dola milioni 280.4 mwaka 2022.

“Tunatambua kuwa makampuni ya Jamhuri ya Korea yamewekeza katika sekta mbalimbali nchini Tanzania, kama vile viwanda, usafirishaji na ujenzi, hivyo kuchangia maendeleo ya nchi zetu. Tunathamini uwekezaji huu,” amesema.

Aidha, Majaliwa alimweleza balozi huyo kuwa aone namna ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata nafasi za kazi nchini Korea hasa kwenye sekta ya uzalishaji.

“Kwa upande wetu sisi tutahakikisha Watanzania wanakuwa na vigezo stahiki vinavyohitajika ili waweze kufanya kazi,” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake Balozi Ju alimweleza Mheshimiwa Majaliwa kuwa katika kipindi chote atakachohudumu kama balozi nchini atahakikisha anasimamia na kuendeleza masuala ya uwekezaji kwa faida ya nchi zote mbili.

spot_img

Latest articles

RC Chalamila tafuta dozi ya Tume Keenja

KATIKA juhudi za kurejesha utawala wa sheria (orderly administration) katika jiji la Dar es...

DAWASA YAANZA MSAKO KWA WANAOJIUNGANISHIA MAJI KINYEMELA

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)...

Vipengele 63 Kuing’arisha The Serengeti Awards 2026

Na Mwandishi Wetu JUMLA ya vipengele 63 vitaingia katika kinyang’anyiro cha The Serengeti Awards...

PSSSF yawajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii

Dar es Salaam- Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha...

More like this

RC Chalamila tafuta dozi ya Tume Keenja

KATIKA juhudi za kurejesha utawala wa sheria (orderly administration) katika jiji la Dar es...

DAWASA YAANZA MSAKO KWA WANAOJIUNGANISHIA MAJI KINYEMELA

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)...

Vipengele 63 Kuing’arisha The Serengeti Awards 2026

Na Mwandishi Wetu JUMLA ya vipengele 63 vitaingia katika kinyang’anyiro cha The Serengeti Awards...