Shilingi Trilioni 8.2 zatumika kukopesha wanafunzi katika kipindi cha miaka 20

Na Mwandishi Wetu 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetumia shilingi trilioni 8.2 kugharamia wanafunzi tangu ilipoanzishwa.

Amesema kuwa pia katika kipindi hicho wanafunzi takribani 830,000 wamenufaika na mfumo huo wa ugharimiaji wa elimu ya juu kupitia Bodi ya mikopo.

Amesema hayo leo Februari 17, 2025 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

“Mafanikio tuliyonayo leo, ni matokeo ya utashi wa kisiasa, uongozi thabiti, maono na michango ya viongozi wetu. Viongozi wetu katika awamu zote walifanya kazi kubwa ya kuhakikisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya vizuri, viongozi wetu walioona mbali kuanzisha mfumo huu wa ugharimiaji wa elimu ya juu kupitia Bodi ya mikopo,” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amesema kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imefanikiwa kukusanya fedha kiasi cha shilingi trilioni 1.5.

“Ninatambua marejesho hayo yamepatikana kutokana na jitihada na ubunifu mkubwa ambao unasaidia kuwafikia wanufaika ambao wamehitimu na mikopo yao imeiva,” amesema Majaliwa.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu haiwi mzigo kwa Wanafunzi, Serikali iliamua kufuta tozo za kulinda thamani ya fedha ili kuondoa changamoto katika urejeshaji wa mikopo.

“Kwa sasa mnufaika anarejesha kiasi kile kile ambacho amekopeshwa kwani tozo hizo zilikuwa zinasababisha ongezeko la madeni ya mikopo hiyo,” Majaliwa.

Ameiagiza Bodi ya Mikopo kuendelea kuweka mikakati ya kuendana na kasi ya mababiliko ya teknolojia na ifanye maboresho ya kujiunganisha na kuzungumza lugha moja na taasisi za fedha nchini. 

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa wakati Rais Dkt. Samia anaingia madarakani alikuta fedha zinazotolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ilikuwa ni shilingi bilioni 464.

“Lakini alipoingia aliagiza fedha kwa ajili ya mikopo ziongezwe, na tuliongeza hadi kufikia bilioni 570, tukaendelea hadi bilioni 654 na sasa ni shilingi bilioni 731,” amesema Majaliwa.

Ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia katika kuhakikisha kada za Sayansi zinaendelea kupewa kipaumbele ili kuzalisha wataalam wengi zaidi, aliiagiza Wizara ya Elimu kutenga fedha kwa ajili ya kuanza kutoa ufadhili kwa ajili ya kada hizo ambayo tuliita Samia Scholarship.

“Wakati tunaanza tulitoa shilingi bilioni 3 kama majaribio, baadae tulitoa bilioni 6 na sasa hivi tumetoa shilingi bilioni 8.9,” amesema.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...