Na Winfrida Mtoi
Kocha Msaidizi wa KMC, John Matambala amefunguka kuwa walipata maumivu makubwa ya kupoteza mchezo ulipita kwa kufungwa na Yanga mabao 6-1, huku akiahidi kijiponya maumivu kwa JKT Tanzania kesho.
Matambala ameyasema hayo leo Februari 17, 2025 wakati akizungumzia maandalizi yao dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja KMC Complex, jijini Dar es Salaam.
Amesema wamejipanda kucheza kama fainali ili kuchukua pointi tatu, licha ya kufahamu ubora wa wapinzani wao.
Kwa upande wake Kacha Mkuu wa JKT Tanzania Ahmed Ally, amesema mchezo huo hautakuwa rahisi kwani kila mmoja anahitaji alama tatu kutokana na nafasi walipo katika msimamo wa Ligi Kuu.