Rais Samia kufanya ziara nchini Ethiopia, kushiriki Mkutano wa Au

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia leo Februari 14 hadi 16 kushiriki mkutano wa kawaida wa 38 wa Nchi na serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga, imeeleza kuwa mkutano huo unatarajia kuchagua mwenyekiti mpya wa AU kwa mwaka 2025 atakayechukua nafasi ya mwenyekiti wa sasa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania.

Pia, mkutano huo pia utachagua viongozi wapya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ikiwemo mwenyekiti, makamu mwenyekiti na makamishna sita.

“Aidha, mkutano huo pia utachagua viongozi wapya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ikiwemo Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna 6.

“Vilevile, Mkutano utajadili Taarifa ya Ushiriki wa Umoja wa Afrika kwenye Mkutano wa Nchi Tajiri Duniani (G20), Utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Taarifa kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi,” imeeleza taarifa hiyo.

Imeongeza kuwa mbali na masuala hayo, Mkutano utajadili Ajenda kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia iliyopendekezwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kabla ya kushiriki Mkutano wa 38, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika utakaofanyika Februari 14,

spot_img

Latest articles

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

Viongozi wa dini waendelea kihimiza amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha...

More like this