Majaliwa aitaka Tarura kuwasimamia wakandarasi binafsi 

Na Mwandishi Wetu 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ihakilishe inatoa kandarasi za ujenzi na ukarabati wa barabara kwa wakandarasi wenye uwezo wa kujenga kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Februari 13, 2025) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Abbasi Tarimba aliyehoji kwanini Serikali isianze kutumia vikosi kazi vya Manispaa au Tarura badala ya wakandarasi binafsi katika ukarabati wa barabara zilizoharibika, katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma.

“Tunaitaka Tarura iwasimamie wakandarasi binafsi wanapopewa kazi, wawe na uwezo wa kujenga barabara za kudumu kwa mujibu wa viwango vilivyopo ili barabara ziweze kutumika kwa muda mrefu,” amesema.

Amesema kuwa awali mfumo wa ujenzi wa barabara za vijijini uliokuwa unaruhusu Halmashauri kukarabati barabara zake ulibaini kuwa na mapungufu hasa kutokana na uwezo tofauti wa kifedha wa baadhi ya Halmashauri.

“Serikali iliwasikiliza waheshimiwa Wabunge ambao wakati wote mlipokuwa mnaomba baadhi ya barabara zenu kwenye Halmashauri zihamishiwe TANROADS, kutokana na maombi ya mara kwa mara tuliamua kuunda Tarura inayoshughulikia barabara za vijijini na mijini na inafanya vizuri,” amesema.

Amefafanua kuwa, Serikali itaendelea kutoa fedha kwa Tarura kwa ajili ya matengenezo ya muda mfupi.

“Tarura tumieni fedha hii vizuri ili kufanya ukarabati kwenye barabara zenye uhitaji wa kukarabatiwa ili ziendelee kutumika,” amesema.

Wakati huohuo, Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya udhibiti wa ugonjwa wa Malaria ikiwemo uendeshaji wa kampeni ya usafi ambayo inagusa pia maeneo yenye mazalia ya mbu.

“Pia tunaendelea na utoaji wa neti kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kujikinga na Malaria,” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa hamasa kwa wawekezaji kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za kutibu ugonjwa malaria na za kupuliza jwenye mazalia ya vijidudu vya Malaria.

“Wengi mnafahamu kuwa pale Kibaha mkoani Pwani tunacho kiwanda cha kutengeneza dawa za kunyunyiza kwenye mazalia ya mbu, Halmashauri sasa zinapaswa kutenga fedha ili kwenda kununua dawa na kunyunyiza kwenye maeneo yote yenye mazalia ya mbu,” amesema.

Akijibu Swali la Mwanaisha Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuwalinda na kujenga ushindani wa wawekezaji wazawa, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imetengengeza mazingira nafuu ya uwekezaji kwa wazawa kwa kupunguza kiwango cha uwekezaji kutoka Dola laki moja hadi dola elfu hamsini.

“Tumeendelea pia kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara kwa wazawa ikiwemo kupunguza kiwango cha kodi kwa bidhaa zinazozalishwa ndani na hata mchakato wa upataji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji,” amesema.

spot_img

Latest articles

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...

TIRDO yasajili Viwanda 25,650, Yaongeza Maabara za Kisasa Kuimarisha Sekta ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya...

More like this

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...