Mwanahabari mkongwe nchini Kenya, Leonard Mambo Mbotela amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Mbotela aliyejulikana kwa kipindi chake maarufu cha Je, Huu Ni Uungwana? amefariki dunia leo Ijumaa saa 3:30 asubuhi.
Akithibitisha kifo cha Mbotela, mke wa mwanaye anayejulikana kwa jina la Anne Mbotela wa mujibu wa amesema kuwa alikuwa mgonjwa kwa muda kabla ya kuaga dunia.

Mbotela alijizolea umaarufu kwa kipindi hicho kilichokuwa kikirushwa na Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC), ambapo alivuta hisia za watu wengi waliokuwa wakimfuatilia.
Kipindi hicho kilianza kuruka mwaka 1966, kikijikita kuhamasisha masuala mbalimbali ikiwemo maadili kimekuwa kikirushwa kupitia Televisheni ya KBC nchini humo.
Kati ya vipindi vyake vilivyopendwa ni Uhalifu Haulipi, Ongea Lugha Sanifu na Waliosifika.