Waziri Chana azitaka Halmashauri zote nchini kulinda wananchi dhidi ya wanyamapori wakali

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana amezielekeza Halmashauri zote nchini kuchukua jukumu la kulinda wananchi dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake.

Ameyasema hayo leo Februari 04, 2025 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu swali la Mhandisi Ezra John Chiwelesa aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuondoa adha ya uvamizi wa tembo katika Kijiji cha Nyabugombe Kata ya Nyakahura – Biharamulo.

“Katika bajeti za Halmashauri asilimia 10 za bajeti za Halmashauri, mapato ya ndani na kuna maeneo Wizara ya Maliasili na Utalii inarudisha fedha za Wildlife Management Areas asilimia 25, fedha hizi zinatakiwa zitumike kwa shughuli rafiki za uhifadhi kulinda wananchi wasiumizwe,” amesisitiza Chana.

Amesema kuwa ajenda ya kulinda wananchi dhidi ya changamoto mbalimbali ikiwemo za wanyamapori wakali na waharibifu ni ajenda ya Halmashauri husika na kusisitiza kwamba halmashauri zina uwezo wa kununua ndege nyuki “drones”, kusomesha vijana kozi za uhifadhi ili wawe Askari wa Vijiji wajue namna ya kulinda wananchi.

Awali akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana na adha ya wanyamapori wakali na waharibifu wakiwemo tembo katika maeneo yanayopakana na Hifadhi ya Taifa Burigi – Chato.

“Mikakati inayotekelezwa ni pamoja na: kuendelea kushirikiana na Wananchi kudhibiti tembo kwa wakati ambapo jumla ya Askari sita (6) wa uhifadhi kwa kushirikiana na mgambo sita (6) waliopewa mafunzo kuhusu tabia za wanyamapori wanatumika kufukuza tembo kupitia kituo cha Nyungwe kilichopo Kijiji cha Nyabugombe, Kata ya Nyakahura” amesema Kitandula.

Kijiji cha Nyabugombe kilichopo katika Kata ya Nyakahura, ni miongoni mwa vijiji 38 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato. Kwa kipindi cha miezi sita Julai – Disemba, 2024 Jumla ya matukio 16 ya tembo yaliripotiwa na kudhibitiwa katika kijiji cha Nyabugombe kilichopo Kata ya Nyakahura, Wilaya ya Biharamulo.

spot_img

Latest articles

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...

Bidhaa ‘feki’ zadidimiza Watanzania lindi la umasikini

Watanzania wanazidi kunasa katika mzunguko wa umasikini unaosababishwa na kushamiri kwa bidhaa duni na...

More like this

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...