Kapinga: Azma ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika wakati wote

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema ni azma ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika na unaotabirika kwa ajili ya shughuli za kijamii na kimaendeleo.

Kapinga ameyasema hayo leo Januari 03, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Lushoto, Shabani Shekilindi aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaondoa changamoto ya kukatika umeme katika Wilaya ya Lushoto kwa kuweka suluhisho la kudumu.

“Tutafuatilia kwa hii wiki moja kufahamu ni nini changamoto ya kukatika kwa umeme Wilaya ya Lushoto, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge iwapo kuna matengenezo tutahakikisha yanakamilika kwa haraka,” amesisitiza Kapinga.

Akijibu swali Mbunge wa Nkasi Kusini, Vicent Mbogo aliyetaka kufahamu uwepo wa nishati ya umeme katika Kijiji cha Msamba-Masokolo, Lyapinda, Izinga na Lyele na katika Vitongoji vya Kisenga na Lupata, Kapinga amesema Wilaya ya Nkasi ina jumla ya vijiji 90 ambapo vyote vimepatiwa huduma ya umeme vikiwemo vijiji vya Lyele na Lyapinda.

Aidha, amesema Kitongoji cha Lupata kilichopo katika Kijiji cha Lyapinda kitapata umeme kupitia mradi wa Vitongoji 15 vya Mbunge utakaotekelezwa na Mkandarasi aitwae M/s STEG International Services Ltd ambaye ameshakamilisha hatua za upimaji na usanifu.

Ameongeza kuwa, uhakiki wa Kitongoji cha Kisenga umekamilika na Kitongoji hicho kitapatiwa umeme kupitia mradi wa vitongoji (HEP IIB).

spot_img

Latest articles

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...

Bidhaa ‘feki’ zadidimiza Watanzania lindi la umasikini

Watanzania wanazidi kunasa katika mzunguko wa umasikini unaosababishwa na kushamiri kwa bidhaa duni na...

More like this

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...