TANZANIA NA SOMALIA KUBADILISHANA WAFUNGWA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI ya Tanzania na Somalia zimesaini mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya ulinzi na usalama na kubadilishana wafungwa.

Mikataba hiyo imesainiwa leo Januari 29, 2025 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Ahmed Moalim Fiqi kwa upande wa Somalia.

Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo, Bashungwa amesema mkataba wa kubadilishana wafungwa utaziwezesha nchi hizo mbili kuruhusu wafungwa waweze kutumikia adhabu katika nchi zao na kusaidia kupunguza gharama za kifedha za kuwahudumia wafungwa hao.

“Inapotokea kuna Watanzania wenzetu wameingia katika hali ya kuwa wafungwa wakiwa kule Somalia, kupitia mkataba tuliosaini utatuwezesha kuwachukuwa Watanzania kuwaleta kwenye magereza yetu, vile vile kwa wafungwa wa Somalia watarudishwa kuendelea na vifungo vyao nchini kwao,” ameeleza.

Aidha, Bashungwa amesema mkataba wa ushirikiano kuhusu ulinzi na usalama, unalenga kuimarisha uwezo vyombo vya usalama kwa kutoa mafunzo kwa Askari wa pande zote mbili, kutekeleza operesheni za pamoja, kubadilishana utaalam katika masuala ya usalama na ulinzi pamoja na kubadilishana taarifa za kiintelijensia.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa amesema utiaji saini wa mikataba hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Somali, Hassan Sheikh Mohamud ili kuendelea kuimarisha ushirikiano.

spot_img

Latest articles

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

Waziri Mkuu ataka kazi za Serikali zifanyike Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inataka kazi zote zifanyike makao...

Mzee Mtei kuzikwa Jumamosi Tengeru

Na Mwandishi Wetu MWASISI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mzee Edwin Mtei anatarajiwa...

More like this

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

Waziri Mkuu ataka kazi za Serikali zifanyike Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inataka kazi zote zifanyike makao...