TANZANIA YAWEKA REKODI MKUTANO WA WAHASIBU WAKUU AFRIKA

Na Mwandishi Wetu

Tanzania imeweka rekodi ya Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika kwa kuwa na washiriki zaidi ya 2000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Serikali Afrika.

Mkutano huo ulioanza  Desemba 2, 2024, ukibeba kauli mbiu ya “Kujenga Imani ya Umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu” uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AIC), umepokelewa kipekee huku ukikusanya Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani na Wataalam wa kada zenye uhusiano wa karibu na uhasibu kama; Wakaguzi wa Hesabu, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA.

Aidha kupitia mkutano huo, washiriki walipata fursa ya kupata ufahamu kutoka kwa wataalam  wa sekta ya umma kuhusu mwelekeo wa kisasa, changamoto, na ubunifu katika usimamizi wa fedha za umma.

Mada mbalimbali zilijadiliwa, kuanzia mabadiliko ya kidijitali katika ufanisi wa sekta ya umma hadi kupambana na mtiririko haramu wa fedha, huku ikitolewa fursa bora za kujifunza ambazo zinaweza kutumika moja kwa moja katika majukumu ya kila siku ya wahasibu na wataalamu wa fedha.


Akizungumza wakati wa Kufunga Mkutano huo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, aliwaasa wahasibu kusimamia taaluma yao kwa kuzingatia misingi ya kitaaluma, na kujiongezea ujuzi ili kuendana na mabadiliko ya
teknolojia.

“Nataka niwaombe wahasibu mtambue kuwa taaluma yenu ni muhimu hata chochote kinachotokea katika sehemu zenu za kazi mtalaumia, hivyo mzuie hasara zinazoweza kutokea” amesema Dkt. Biteko.

Naye Naibu Waziri wa Fedha,  Hamad Hassan Chande, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha,  Dk. Mwigulu Nchemba, aliwataka wahasibu wote Barani Afrika, kuwa waaminifu na kuzisaidia nchi zao katika kuhakikisha zinapata maendeleo.

Alisema kuwa kazi zozote zinazofanywa hususani za miradi ya maendeleo katika nchi za Bara la Afrika zinawahusisha wahasibu hivyo, wazingatie maadili ya taaluma zao na miongozo inayotolewa katika nchi zao ili kuhakikisha malengo yanayopangwa yanafanikiwa.

spot_img

Latest articles

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

Simba yainyuka Fountain Gate mabao 3-0

Na Mwandishi Wetu  SIMBA imechukua alama zote tatu kwa Fountain Gate kufuatia ushindi wa 3-0...

Mahakama yaipa uhuru Chadema, sasa ruksa kufanya siasa

Na Mwandishi Wetu MAHAKAMA ya Rufani Tanzania leo 15 Aprili 2026, imekiondolea kifungo cha kutofanya...

More like this

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

Simba yainyuka Fountain Gate mabao 3-0

Na Mwandishi Wetu  SIMBA imechukua alama zote tatu kwa Fountain Gate kufuatia ushindi wa 3-0...