MAJALIWA- RAIS SAMIA AAGIZA FEDHA ZA MAADHIMISHO YA UHURU ZIELEKEZWE KUTOA HUDUMA ZA KIJAMII

Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka 2024 yafanyike katika ngazi ya mikoa na Fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii.

Amesema kuwa kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile kwenye Masoko, Hospitali, Kambi za wazee na wenye mahitaji maalum, mashindano ya michezo mbalimbali pamoja na makongamano na midahalo ya kujadili maendeleo endelevu ambayo nchi yetu imefikia katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru.

Amesema hayo leo Jumatano Desemba 04,2024 katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. “Sherehe za Mwaka huu hazitakuwa na Gwaride na Shughuli nyingine za Kitaifa”.

Amesema kuwa Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu. “Ninatoa rai kwa Wakuu wote wa Mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo Mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa shughuli za Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya Mwaka 2024 zilishaanza tangu Desemba 02 na zitafanyika mpaka 09 Desemba, 2024 Siku ya kilele.

“Katika maadhimisho haya, Taasisi zote za Serikali na Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama zinaelekezwa kuhakikisha Majengo yote ya Serikali Tanzania Bara yanapambwa kwa vitambaa vya rangi ya Bendera ya Taifa, picha rasmi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni Muasisi wa Uhuru wetu pamoja na picha ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema.

Kauli Mbiu inayosema, Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara: “UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI MSINGI WA MAENDELEO YETU.”

spot_img

Latest articles

Serikali: Tuchukue hatua kuepuka madhara ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA)

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia kwa Mkurugenzi msaidizi, Kitengo cha Afya Moja, Ofisi ya...

Serikali yawaita wadau kujitokeza kusapoti ushiriki wa wanawake michezoni

Na Winfrida Mtoi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' amewaomba...

Ndejembi awahakikishia wakazi wa Kigamboni umeme wa uhakika

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ndani ya...

Viongozi Chadema washinda shauri la kuidharau Mahakama

Na Mwandishi Wetu Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali shauri la maombi...

More like this