Ramovic awaita mashabiki uwanjani, anapenda kuitwa Tanzanian Machine

Na Winfrida Mtoi

Kocha Mkuu wa Yanga,Sead Ramovic amesema mashabiki wanamuita ‘German Machine’ lakini yeye angependa kuitwa ‘Tanzanian Machine’, huku akiwaita mashabiki wa timu hiyo kesho kujitokeza uwanjani ili kukaribisha na kumsapoti ili kupata matokeo mazuri.

Yanga kesho Novemba 26,2024 inashuka dimbani kucheza na Al Hilal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika  kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.  

“Mashabiki wananiita German Machine, lakini mimi ukiniuliza ningependa kuitwa Tanzanian Machine, nataka kufurahi pamoja na watu wa hapa na kuhakikisha klabu hii inapata mafanikio,” amesema Ramovic.

Aidha amesema Yanga ni timu bora lakini pia wanakwenda kucheza na timu bora, hivyo wanahitaji umakini kukabiliana na mchezo huo mgumu.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa. Ni jambo la kheri sana kwangu kushiriki mashindano haya makubwa nikiwa na timu kubwa. Falsafa yangu kubwa ni nidhamu na kujituma. Napenda kuona wachezaji wakicheza kama timu, haijalishi unatumia mfumo gani kama wachezaji wako hawana umoja ni ngumu kupata matokeo,” ameeleza.

Kocha huyo amesema katika timu yao hakuna mtu ambaye ni staa kwa sababu kila mtu ni staa ndani ya kikosi hicho.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Bakari Mwamnyeto amesema anajua kwamba mechi ya kesho itakuwa ngumu lakini wapinzani wao wajipange kwani wasipoangalia wanaweza kula hata goli tano.

spot_img

Latest articles

Serikali yaahidi kushirikiana na wadau kuendeleza mchezo wa kuogelea

Na Winfrida Mtoi WADAU wa mchezo wakuogelea Afrika Mashariki wamekutana kujadili maendeleo ya mchezo huo,...

Dube awapa raha wananchi

Na Winfrida Mtoi BAO pekee lililofungwa na Prince Dube dakika ya 58, limeipa Yanga alama...

Mexico yatwaa taji la Miss Universe 2025, Ivory Coast namba tano

Na Mwandishi Wetu Mexico imeibuka mshindi wa taji la Miss Universe 2025 kupitia mrembo wake...

Kocha Yanga ataja mbinu kuingamiza FAR Rabat

Na Mwandishi Wetu KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Concalves amesema falsafa yake katika mechi ya...

More like this