Dk. Biteko asisitiza kupiga kura ni haki ya Kikatiba

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewahimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Dk. Biteko ametoa rai hiyo leo Novemba 25,2024 akiwa mkoani Geita ambapo amesema uchaguzi huo ni muhimu hususan kwa ukuzaji wa demokrasia nchini.

“Naomba Watanzania wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika maeneo yao wajitokeze kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wao,” amesema Dk. Biteko.

“Viongozi hawa ndio msingi katika nchi yetu, viongozi hawa ndio wanajua watu wanaishije, wana shida gani na watafanya nini kutatua shida hizo. Ni muhimu wote kushiriki kuchagua viongozi tunaowataka,” amesisitiza.

Aidha, Dk. Biteko amebainisha kuwa kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa hivyo watu wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura ifikapo Novemba 27, 2024.

spot_img

Latest articles

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu  SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini...

More like this