King Kikii afariki, Rais Samia amlilia

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kutokana na kifo cha mkongwe wa muziki wa dansi,  Boniface Kikumbi ‘King Kikii’ na kusema nguli huyo atakumbukwa na kuenziwa   kwa kazi zake nyingi nzuri ikiwamo wimbo wa kitambaa cheupe.

Amesema King Kikii ametoa burudani kwa mamilioni ya Watanzania na amekuwa mlezi na mwalimu wa wengi katika tasnia ya muziki.

“Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wasanii na wapenzi wote wa muziki nchini kufuatia kifo cha mwanamuziki nguli Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’.

Kwa zaidi ya miaka 50 King Kikii. Tutamkumbuka na kumuenzi kwa kazi zake nyingi na nzuri ikiwemo wimbo wake maarufu wa ‘Kitambaa Cheupe’ ambao umeendelea kuwa sehemu ya burudani kwenye maeneo na shughuli mbalimbali za burudani nchini.

“Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema”

King Kikii amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 15, 2024 nyumbani kwake Mtoni kwa Aziz Ally, jijini Dar es Salaam.

spot_img

Latest articles

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

Waziri Mkuu ataka kazi za Serikali zifanyike Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inataka kazi zote zifanyike makao...

Mzee Mtei kuzikwa Jumamosi Tengeru

Na Mwandishi Wetu MWASISI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mzee Edwin Mtei anatarajiwa...

More like this