Na Mwandishi Wetu
Wachezaji wa timu ya Simba, viongozi na benchi la ufundi wamekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Septemba 25,2024 baada ya kuwasili visiwani humo kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Azam utakaochezwa Uwanja wa Amani Complex.
Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu Zanzibar, Simba wamemkabi zawadi ya jezi Rais Dk. Mwinyi pamoja na mke wake mama Mariam Mwinyi.
Akizungumzia katika hafla hiyo, Rais Mwinyi ameipongeza kutokana na kuiwakilisha vyema kimataifa kwani jambo hilo linasaidia kukuza utalii kupitia michezo.
Pia Rais huyo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sinajipanga kujenga uwanja mkubwa wa michezo utakaokuwa na vigezo vinavyokubalika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha michuano ya soka inayowashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) na ile ya michuano ya soka ya mataifa ya Afrika kwa timu za taifa (AFCON), kuwa Zanzibar ni sehemu itakayochezwa michezo hiyo.
Ameelezea dhamira ya Simba ya kujenga kituo cha kuwaendeleza vijana katika mchezo wa soka hapa Zanzibar (soccer academy) kuwa ni jambo jema na kuwaahidi Serikali ipo tayari kuwaunga mkono kwa kuwapa eneo la ujenzi wa kituo hicho.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha michuano ya soka inayowashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) na ile ya michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika kwa timu za Taifa (AFCON), kuwa Zanzibar ni sehemu itakayochezwa michezo hiyo.