Wenye migogoro ya bima waitwa kusuluhishwa

Na Mwandishi Wetu

Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, Margaret Mngumi amewataka wananchi wenye changamoto za madai ya bima kutembelea Kijiji cha Bima kilichopo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) waweze kutatuliwa.

Akizungumza Julai 7,2024 na Waandishi wa habari, amesema ofisi hiyo inalenga kutatua migogoro ya bima kwa njia mbadala yaani nje ya utaratibu wa kimahakama na kusuluhisha kwa gharama nafuu na haraka.

Amesema wanasuluhisha migogoro baina ya wateja wa bima dhidi ya kampuni za bima ambazo zimesajiliwa kufanya biashara ya bima.

“Mwananchi anapokwenda kudai fidia ya bima kwa kampuni ya bima iwapo hataridhika na namna ambavyo wanashughulikia madai yake, waje ofisi ya msuluhishi wa migogoro ya bima ili tuweze kutatua mgogoro husika.

“Migogoro ambayo inasuluhishwa ni ile ya viwango vya fidia ya bima, eneo lingine la migogoro linatokana na tafsiri sahihi ya mkataba wa bima, mara nyingi mteja na kampuni ya bima wanakuwa hawaelewani juu ya tafsiri sahihi ya mkataba,” amesema Mngumi.

Amesema wanatumia maonesho ya mwaka huu kutoa elimu na kusuluhisha migogoro kutoka kwa wadau mbalimbali na kuwataka wananchi kutembelea Kijiji cha Bima kilichoko ndani ya maonesho hayo ambako kuna banda la msuluhisi wa migogoro hiyo.

Mwakilishi wa Kampuni za Bima zinazoshiriki maonesho ya Sabasaba, Alilya Kwayu, amewashauri Watanzania kujenga utamaduni wa kukata bima kama za afya, nyumba, magari, elimu, maisha ili iwe ziwasaidie pindi wanapopata majanga mbalimbali.

“Katika maonesho haya tunawaelimisha Watanzania kuhusu huduma za bima zenye uhakika, bima ina faida inasaidia kuchangia mfuko ambao unaweza kulipa kidogo kidogo na ikitokea mtu mwingine akapata majanga anarudi katika hali yake,” amesema Kwayu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya Bima ya Bumaco.

Kwa upande wake Meneja Uandikishaji kutoka Kampuni ya Bima Mtawanyo (Grand Reinsurance), Charles Chanya, amesema wanatoa huduma kwa makampuni ya bima kwa lengo la kuyaongezea uwezo katika shughuli zao za kila siku.

“Kampuni za bima huwa zinafanya biashara ambazo pengine inaweza kufikia hatua zinazidi uwezo, yanapozidiwa uwezo yanakuja katika kampuni za bima mtawanyo kuomba kuongezewa uwezo ili kuandikisha bima zaidi…tunaongeza uwezo wa kifedha lakini hatuwapatii fedha, wanaandikisha bima kwa kutumia mtaji wetu,” amesema Chanya.

spot_img

Latest articles

Maboresho ya mitambo ya kufua umeme Mtera yaimarisha uzalishaji umeme

Na Mwandishi Wetu, Mtera NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Novemba 26, 2025, alitembelea na...

Ndejembi: Tanzania sasa ina umeme wa kutosha

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Tanzania kwa sasa ina umeme...

Jeshi la Polisi lachunguza  taarifa ya OCD  Chunya

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi limesema limeona na linafanyia uchunguzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao...

Uwanja wa Mkwakwani wafungiwa

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeufungia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutumika kwa...

More like this

Maboresho ya mitambo ya kufua umeme Mtera yaimarisha uzalishaji umeme

Na Mwandishi Wetu, Mtera NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Novemba 26, 2025, alitembelea na...

Ndejembi: Tanzania sasa ina umeme wa kutosha

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Tanzania kwa sasa ina umeme...

Jeshi la Polisi lachunguza  taarifa ya OCD  Chunya

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi limesema limeona na linafanyia uchunguzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao...